Habari za leo wanajamiiforum,
Nina shost yupo nchi za ughaibuni, anataka kusoma kati ya unesi au medical laboratories.
Ila bidada anataka akisha soma arudi zake bongo kufanya kazi. Mimi kwa ushauri wangu nimemwambia
bongo unesi haulipi, labda hiyo medical laboratories, ila nayo sijui kama inalipa hapa bongo au lahh!!
Maana sina uzoefu nayo. Hivyo nipeni ushauri wa kina ipi itamfaa bidada akija hapa bongo. Mwenyewe
hataki kabisa kuishi ughaibuni, anataka apate elimu na arudi zake bongo.
Haya wanaojua toa ushauri, ili nimfikishie mlengwa.