Ushauri unahitajika kwa dada yetu

Nyatyo

Member
Joined
Sep 21, 2017
Posts
89
Reaction score
78
Admin mimi nimeolewa na nina mtoto mmoja wa kiume. Kabla sijaolewa nilikua na mahusiano na kijana wa Kichaga, kiukwel tulipendana na yule kijana alinijali, aliniheshimu, kiufupi tuliishi vizuri mikwaruzano ilikuwa michache sana.

Kipindi hicho nilikuwa sina ajira, bali nilikua nafanya kazi ya kujitolea kwenye taasisi fulani, ila huyo kijana yeye ni mwajiriwa wa serikalini. Tulifanikiwa kufungua duka, kiukweli duka lilikua linaenda vizuri.niliwaza huyu ndie atakuja kua mume wangu lkn haikua hivyo.

Tulikuwa na ukaribu hatua hadi nyumbani kwao nilifahamika, na yeye alifamika kwa baadhi ya ndugu zangu ila siyo wazazi na tangu nimekua naye mambo yalikua vizuri, kiufupi nilienjoy mapenzi yake kwa kipindi chote hadi pale nilipoanza kuwasiliana na rafiki yangu mwingine ambaye kwa sasa ni mume wangu.

Huyu kijana (name hide) alikua rafiki tu, tuliambiana mambo mengi na kushauriana, sikuwahi kukutana naye kimwili, alikua rafiki tu. Ghafla huyu kijana akaniambia kuwa anataka kunioa, kiukwel nilidhani masihara lakini kadri siku zilivyozid niliona inakua 'serious'. Niliongea na mpenzi wangu Mchaga nikamwambia habari za kuoana akaniambia nisubiri nimalize shule sababu nilikuwa nasoma chuo halafu ndiyo tutanza hizo taratibu.

Lakini pia alikua ananisisitiza nimzalie mtoto kwanza, kiukweli tulipishana maana anataka nimzalie mtoto kabla ya ndoa, nikimwambia swala la ndoa anasema mpaka nimalize chuo upande wangu niliona haijakaa poa.

Sasa wazo la rafiki yangu la kutaka kunioa likaanza kuniingia kichwani. Sijui ni nini kilipata nikaanza kutamani ndoa hadi inafikia hatua tunagombana na Mchaga wangu swala la ndoa.

Hiyo siku niliongea na rafiki aliyetaka kunioa akaniambia amenipenda na ananijua muda mrefu hivyo anaona ninamfaa kuwa mke wake. Akaniambia tupime afya kiukwel nilifanya hivyo bahati nzuri afya zetu zilikua vizuri, na hakuchelewa ikabidi apeleke posa nyumbani, wazazi walipokea na kufanya mandalizi ya kujibu posa.

Kiukwel nilikua na wakati mgumu maana nilimpenda sana Mchaga. Siku moja ilibidi nimwambie Mchaga kuwa nyumbani kuna mtu ameleta posa na bado haijajibiwa, yule Mchaga alikasirika akaniambia kuwa nilikua na mahusiano mengne wakati nipo na yeye jambo ambalo siyo kweli.

Kwahiyo alijibu kwa hasira akaniambia kama unataka kuolewa olewa na kama utanisubiri sawa. Binafsi lile jibu sikulipenda na hapo ndiyo nilipowaza kua Mchaga alikuwa ananichezea tu, hana haja na mimi. Ilibidi niwaambie wazazi wajibu kuwa nipo tayari kuolewa, wazazi walifanya hivyo na ikawa inasubiriwa tarehe ya mahari.

Kipindi yote yanafanyika bado nipo na Mchaga hatujaachana na tangu anijibu vile hatukuwai tena kuzungumzia hilo swala, hivyo nilikuwa nafanya mambo yangu kimya kimya bila yeye kujua. Tarehe ya mahari ilipangwa tukaenda, ni nje ya mji hivyo nilimdanganya Mchaga kuwa naenda kusalimia nyumbani kumbe naenda kutolewa mahari.

Niliporudi tu nilionana na Mchaga, kiukwel nilimuona hayupo sawa kabisa. Kwanza alikuwa kapungua, nikamuliza shida nini akasema hakuna shida ila anahisi homa. Pia nilikua natafuta namna ili tuachane niendelee na mambo ya ndoa.

Siku iliyofuata alikuwa kazini akanipigia simu sikupokea siku nzima, iliniuma lakini nilikua natafuta namna achukie tuachane. Kweli siku iliyofuata tena akapiga sikupokea, akatuma ujumbe kuwa nipokee ana jambo la muhimu hapo nikapokea simu yake.

Kiukwel aliongea maneno makali sana, akasema anajua kila kinachoendelea na ana namba hadi ya huyo bw. harusi mtarajiwa na akanitumia baadhi ya sms tulizokuwa tukichat na bw. harusi mtarajiwa na akaniambia niendelee na mambo yangu kamwe sitokuja kufurahia ndoa. Kiufupi aliongea maneno mabaya na vitisho juu, alipaniki sana na ndiyo siku tuliyovunja uhusiano wetu.

Niliolewa na Mungu akatubariki mtoto. Mwanzoni nilifurahia sana ndoa lakini hivi sasa naona majuto. Mwanaume amebadilika sana, kwanza anataka aoe mke wa pili, cha pili nimefatilia nyendo zake ni mtu mwenye mambo mengi hasa ya wanawake, ni muongo na tangu tumefunga ndoa hakuna mafanikio yoyote tuliyopata zaidi ni kupoteza na kwa upande wangu mambo yamekua hovyo sana.

Kuna muda najitahidi kuvumilia lakini roho inaniuma sana na inanipelekea namkumbuka Mchaga. Siku moja nilijaribu kutuma ujumbe namba ya Mchaga, kiukwel ilikua hewani na alijibu na kunipigia. Tuliongea sana na nilimuomba msamaha nikamwambia nikwel nilimkosea lakini asiwe na kinyongo na mimi.

Nilimbembeleza sana akaniambia ameshanisamehe lakini bado hajanisahau, tukawa tunawasiliana tu kama marafiki. Lakini kadri vituko vya mume vinavyozidi namtafuta Mchaga, kiukwel ananifariji ikafika mahala nilimweleza kuwa mambo siyo mazuri.

Alihuzunika na akaniambia anaomba turudiane hata kama nimeshazaa. Pia akaniambia mimi nina nguvu ambayo inampa mafanikio kwahiyo akiwa na mimi mambo yake yanaenda vizuri. Siku moja ilibidi nikutane naye na tulikaa sehemu tukaongea kwa kirefu sana na hatukufanya chochote japo alinilazimisha sana.

Kiukweli pamoja na yote yanayoendelea sijawahi kumsaliti mume wangu, Sasa hivi karibuni Mchaga alifiwa na bibi yake ambaye ninamfahamu, ilinibidi niende msibani. Nilifanikiwa kuonana na ndugu zake, kiukweli bado wananipenda.

Pia na lile duka tulilofungua bado lipo, baada ya msiba Mchaga alinipigia simu akaniambia anataka anioe. Hivyo akaniambia kwakua mume wangu anataka kuongeza mke wa pili, nitumie hiyo kama fursa ya kuvunja ndoa ili anioe yeye na akarudia tena kusema akiwa na mimi mambo yake yanaenda vizuri. Japo hapa kati tulivyopotezana alishakuwa na mahusiano lakini hayajadumu.

Kwa sasa nipo njia panda sielewi. Nawaza je, anania kweli ya kunioa au anataka alipize kisasi? Kwasabu ni haraka sana anataka hili jambo. Na je, ananipenda kweli au anatumia ushirikina maana anasema mimi ndiyo nguvu yake ya mafanikio. Naogopa na sielewi nifanye maamuzi gani, nipo njia panda, au nibaki tu kwenye ndoa nivumilie labda atakuja kubadilika?

Nimelileta kwenu naomba ushauri, nipo njia panda nashindwa kufanya maamuzi, ninachotaka niwe na furaha.
 
Uko na ujinga mwingi saana...sasa hata kama haujipendi wewe hauonei huruma hiyo sehemu yako ya siri na watoto unaowazaa?

unafunga ndoa huku....unazileta familia mbili zenye watu waliokuzidi umri huku haujui unataka nini....

Haujaja duniani kuruka hapa na hapa....Una watoto wanaohitaji kutengenezewa future na kuyapata mapenzi ya baba na mama.

Uko na ujinga mwingi saana.
 
Mwandiko wako mbaya Sana
Hujui hata matumizi ya R na L
A na H then unasema umesoma chuo?

Kiufupi wewe ni wale mademu wa kuokoteza wenye Akili za kimasikini na chuki na Gundu
 
Binafsi nimeshindwa kusoma.. uandishi unaumiza macho

Sent from my SM-A135F using JamiiForums mobile app
 
Unajua mwanamke akiambiwa anataka kuolewa basi akili yake Inakuwa inaenda haraka kwamba hasikii wala hambiliki.. naona kwa jamii ya sasa unaweza kuishi na jmaa mkaenjoy life na ushaingiza mambo ya kishirikina sijui anakutumia izo ni imani potofu hakuna kitu kama icho ...hapo karma imechukua nafasi may be huyo mchaga alitaka kuweka mazingira mazuri zaidi ya nyie kuoana ila wwe una haraka sana...

Na kuhusu ishu ya mwanaume kuwa na wanawake wengi ni japo la kujipendekeza tu ..hapo umepatika kwamba tukiongea uhalisia akishakuzalisha ni kuwa hauna maajabu anatafuta mwanamke mwingine so jipange...yeye kakuchunguza ndo maana akakuoa ila wew haujamchunguza inawezekana huyo mchaga unamjua vizuri kuliko huyo uliyekurupuka kuolewa nae.
 
Sasa wewe unajua kabila la mwanaume mmoja tu wa kichaga, huyo mungine haulijui kabila lake?

Mbona mada yako imehusisha sana swala la kabila kuliko ulichokusudia kuandika.
Kila hatua mchaga... kila hatua mchaga... Bora hata ungeandika jina lolote na ukasema kwamba umeamua kutumia jina hilo kwa sababu ya kuficha jina lake halisi. Kuliko uzi mzima mchaga mchaga, ila huyo mungine haukulitaja kabila lake.

Anyway ngoja nimalize kusoma afu narudi tena kuangalia kama kuna namna yoyote ya kukushauri.
 
Nimesoma sentence 2 kumbe ningeendelea mzigo ulikuwa mkubwa hivi duh 🍻
 
Usipokuwa mwangalifu utakula 10 za kichwa. Haya. Shauri yako- Ni ushauri tu.
 
Kinachoshangaza zaidi, mmwanaume mmoja anamtaja kwa kabila lake mwingine hasemi kabila lake na wala yeye hajajitambulisha ni kabila gani.....

Weird.....
 
Una kiranga mwanamke naona tu hapo umekumbuka ukunaji wa bwana mchaga na huenda ana vijisenti so umemtafutia sababu mumeo ili u justify unachotaka kukifanya. Tulia mwana wa kike hata huku unakotaka kukimbilia utajutia sana. Hakuna ndoa rahisi kamwe so usije ona ugumu kwa hii ya kwanza ukadhani ya pili uta enjoy.
Tulia kwanza jipe muda, nimechoka kuandika😴
 


Mleta Mada Andika Vizuri Acha Kurundika Mwandiko Wako Mpaka Unakosa Mvuto Wa Kusoma!!

 
Un
Una umri gani?yaani wewe tikiti maji kabisa...yaani sifuri
 
Umenikumbusha dah!Nilishasahau.ELIZA ulaaniweeee!
 
Usikosee mara mbili, chunga, heshimu na baki na ndoa yako.
 
Hawa viumbe achana nao.
Ukiona una mpenzi na malengo ya kuoana akaanza kukuliza hivi unakuja lini kujitambukisha au unampango gani ujue ana plan B.
Hawanaga uvumilivu.
yakimshinda anakukumbuka.
ndivyo walivyo hawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…