Ushauri unahitajika: Mabati ya plastic

Ushauri unahitajika: Mabati ya plastic

Lububi

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2013
Posts
2,158
Reaction score
3,808
Wachina wameleta mapinduzi ya uezekaji kwa aina mpya ya bati za plastic na sifa kedekede kama kupoza nyumba, kurecycle yakichakaa, uimara, kutovuja kupitia misumari, bei ndogo, kutunza hewa safi na kutokuwa na kutu. Warranty ya miaka 30.

Tena wanatengenezea hapa nchini, hili jukwaa limesheheni wataalam. Anayejua uhalisia wa ubora na uimara naomba msaada wake. Kwa lugha tu ni mabati yanayoshawishi kutumia.

179125967_199615908644716_170171588800883531_n.jpg
 
wachina wameleta mapinduzi ya uezekaji kwa aina mpya ya bati za plastic na sifa kedekede kama kupoza nyumba, kurecycle yakichakaa, uimara, kutovuja kupitia misumari, bei ndogo, kutunza hewa safi na kutokuwa na kutu. warranty ya miaka 30. tena wanatengenezea hapa nchini. hili jukwaa limeshehen wataalam. anayejua uhalisia wa ubora na uimara naomba msaada wake. kwa lugha tu ni mabati yanayoshawishi kutumia.

View attachment 1767807
Inaonekana unajua abc zake...FANYA UTARATIBU TUWEKEE NA BEI KABISA,TUJIPANGE...NINA KAJUMBA KAKUEZEKA MUDA SI MREFU
 
Haya yatavumilia KUPIGWA na jua Kali la DODOMA kweli?
 
Tupatie details zake
Ubora wake
Faida zake kulinganisha na bati za kawaida
Bei
Zinafatikana wapi
 
Tujiulize hivi... Ikitokea ajali ya moto na bati ni hizo plastic, majanga yatakua makubwa au madogo?

Usalama kwanza!

TBS, TBS, TBS... Nawaita mara tatu.
 
Yametumika nchi gani tupate experience yao?...warranty achana nayo kwa sasa..wanakua wasumbufu hao mambo yakoharibika
 
Nilienda dukani nikayakuta kwa gharama ya elfu 9 tu kama kumbukumbu zangu hazijaenda likizo bado.. Almanusura ninunue kwa akili ya ubahili lakini nilivyomeza mate ya akili, akili ya kikubwa ikaniambia hiyo ni kamari nikaachana nayo.
 
Mbona yako kitambo si yale meupe translucency yanaitwa sema now yameleta rang nying nying
 
Back
Top Bottom