Ushauri unahitajika nifanye kipi kati ya haya?

Ushauri unahitajika nifanye kipi kati ya haya?

Optimists

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2021
Posts
379
Reaction score
1,082
Wakuu habari!

Niende moja kwa moja kwenye mada husika. Humu kuna watu wana experience walishafanya au bado wanafanya itasaidia kwa namna moja au nyingine. Niko na idea mbili tatu sijajua nifanye hipi naomba mnipe msaada wa mawazo kutokana na experience yenu.

Niko na mtaji kidogo wazo langu la kwanza nichukue balo la mtumba nifungulishe lakini nikashauriwa kwamba sina uzoefu nitapoteza ndio likaja wazo la "kupoint nguo" na idea ya kufanya nguo za kike na watoto niuze kuzunguka kwenye minada around Dar.

Wazo jingine ni kwamba nichukue vitu kwa bei rahisi kutoka kariakoo either nguo za special au vile viatu vya kike au phone accessories then nizunguke minadani nje ya Dar.

Kipi ni bora kati ya hivyo? Je, minada gani nje ya Dar itanisaidia kwenye mzunguko na kuikuza hela?
Napokea ushauri DM

Shukrani
 
Point nguo hizo ulizozitaja hapo peleka minadani Kama utaweza ucheze na social media ..au waweza tembeza na mitaani pia... Mdogo Mdogo ukishakomaa katika mtaji Rudi Sasa kwenye kufungulisha mabalo.

Yangu hayo tu..😊
Shukrani.
Mtaji wa kufungulisha balo ninao changamoto ni uzoefu maana nimeambiwa naweza tumia 1.2 million kufungua balo mbili au tatu then nikapata laki 8
 
Kwa nguo za special sikushauri maana hizo hua zikitoka after few weeks zinapotea kwa fashion zinakuja zingine.

Kama unauza kwa mnada best option ni kununua balo sababu ukipoint itakulazimu uuze kwa bei ya juu kiasi of which haitafaa sababu minada mingi nguo bei chee.

Fatilia wauzaji mabalo ambao atleast wanaeleweka au utafute mtu mwenye uzoefu akuelekeze kwa supplier ambao ni wa uhakika na wenye nguo nzuri kutokana na budget yako.
 
Asante sana
 
Kabla ya kuanza kwenda mikoani, tembelea minada ya Dar, note down kila mnada unafanyika siku gani, muda gani huo mnada ndio unakuwa na wateja, gharama za kupata meza au sehemu ya kuuzia, bidhaa gani zinatoka sana kwenye hio minada, gharama za usafiri, store ya bidhaa zako nk
Anza kwa ku point nguo nzuri unazozipenda unazoamini zinaendana na minada uliyopitia alafu anza biashara, in 6 month InshaAllah utakua mzoefu, utakua na connection za kununua ma balo mazuri ambayo utauza kwa bei rejareja na jumla kwa wateja wako.
 
Back
Top Bottom