huyo baba kazidi kama ni mm kwavile nimempenda binti sharti la kwanza ningekubali ila nikishaoa babamkwe stop kunipangia nn cha kufanya na nn nisifanye kwani mtu atamwacha babae na ***** na kuambatana na mumewe huyo binti bado ajawaacha wa kwao ataukimwoa atakusumbua kwani kila utakacho mwambia lazima akasililize ushauri wa baba alafu atakwambia babakasema
Swala dogo.
Kukata mzizi wa fitina wote waachane na dini zote, wawe hawana dini, na ndugu yeyote atakaye wa mind waue undugu.
Kwanza mungu mwenyewe hayupo na ndugu wengine mzigo mtupu.Kama mtu anaweza kukumind katika maamuzi yako mweyewe kiasi hiki huyu si ndugu ila ni mkoloni anatak kuku control tu.
Kama wanataka kuishi bila complication ndiyo hivyo, ndoa kwa mkuu wa wilaya, mtoto habatizwi kwa moto wala maji, period.
Kwisha kazi, kata mzizi wa fitina, kaput.
Hapo kuna mengi ya kutafakari, hawa wazee wakati mwingine wanapotoka. Kuna mzee mmoja amekataa kumuozesha binti yake kwa visingizio kibao, mara tunda la kuvundika si sawa na la kuivia mtini akimaanisha hata kijana akikubali kubadili dhehebu bado asingefaa maana kijana ni mkatoliki na binti ni msabato. Sasa binti ana watoto 3 bado yupo kwa baba ake... watu wanajiuliza ni kweli dhehebu linaweza kusababisha yote haya au mzee ana agenda ya siri na binti yake?
Annina
........Huyu msichana hana msimamo, dhehebu sio kigezo kabisa hapa. Wangapi wameona madhehebu tofauti na bado ndoa zao ni paradiso ndogo hapa duniani. Kama kweli angekuwa na msimamo angemwambia ukweli baba yake kwamba atafunga ndoa kwenye dhehebu la huyo mwanaume na kuendelea na hilo dhehebu................mimi sioni kikwazo hapa, binti anatakiwa kuwa na msimamo kama kweli anampenda huyo kijana ili wafunge ndoa.
huyo baba naye anamatatizo ..kama wote ni wakristo kuna tatizo gani hapo?
na huyo baba hajui maandiko yasemayo mwanamke ataacha wazazi wake na ataambatana na mmewe nao watakuwa mwili mmoja
Swala la watoto ni juu ya Baba na mama kuamua wasali na sio babu yao
kaniuzi huyo baba mkwe ..Binti nae ka msimamo kake kako 50/50% Y
Kitendo cha huyo dada kusema kuwa kama ikishindikana basi waachane, ni ishara tosha kuwa upendo wa huyo dada kwa huyu ndugu yetu ni wa mashaka sana. Na sidhani kama ni legible candidate wa kula kiapo cha kuishi na huyo jamaa siku zote za maisha yao na kuwa hakuna kitu cha kuwatenganisha isipokuwa kifo tu!!!!. kwani hata huyo bwana akikubali inaweza kutokea jambo lolote lile ambalo ni upendo wa huyo dada pekee ndo utakao determini whether hiyo ndoa iendelee au la, na kwa upendo duni alionao huyo dada bila shaka hiyo ndoa itavunjika tu.
Unaweza kuwa ni ushauri mgumu sana kuukubali huyu bwana, lakini tusije tukaharibu kwa kutoa ushauri utakao mfurahisha tu huyu bwana. Mimi nakushauri sitisha hilo zoezi kwanza na kuu evaluate upendo wa huyo dada kwako. Ukishadhibitisha kuwa kweli anakupenda, na hakuna kitu wala mtu (e.g Baba, mama, kaka, jirani n.k) anaeweza kuwatenganisha wawili nyie isipokuwa kifo, then anza tena mchakato. Ukiprove otherwise achana nae kuepusha potential frustrations ahead.
Tafakari, chukua hatua.
Mwambie ambebe mchumba wake, mguu kwa mguu wende kwa baba yake amwonyeshe malezi ya dini aliyomlelea binti yake yamemfikisha wapi, kisha ampe muda huyo binti kwa hiyari yake aamue kuolewa na dini anayotaka. Kumlazimisha huku anamimba ataolewa na kinyongo, afu ndo wale wakipata PhD kwasababu anajua hata baba yake hahuifurahia hiyo ndoa anaishia na watoto. Binti awe na msimamo.
eeeeh! hapo kweli mambo mazito, anaweza kuingia kwenye matatizo makubwa, mi ningeshauri apate muda wa kutafakari zaidi jambo hili pamoja na huyo bibie, wazazi wengine bwana! anatema biti kwa mshenga khaah! subiri apate habari ya kuwa bintiye kamimbika kama hajawa mpoleKwa kweli hili pia na mimi lilinishtua....! Kutokana na msimamo huo hata mshenga amerudi nyuma anataka kujitoa....manake baba mkwe msimamo wake uko hivyo na ameshamwambia mshenga asirudi kwake kama hawajakubaliana na hayo.
Hapo sijaona udini wala udhehebu. Huyo dogo anataka kuoa mchawi ila hajui tu. Kusaini kiapo cha nini vile??? Hayo ndo madogoli live....welcome to withcraft society...ndo hao wanaogombea maiti.
We chukua mzigo....huyo dingi hafai kusikilizwa..hiyo ndoa haimuhusu kihivyo ..anavuka mipaka sasa ebo!!
hii si kitu ya juu juu
Bolded -
-kwa nini binti anakubaliana na baba yake?
-mimba ya miezi mitano baba wa binti hajang'aka?
- nasikia kuna koo na jamii zingine huwa kama zimelaanika hivi, unaoa lakini angalau nusu ya watoto unaodai ni wako, kiuhalisia si wako wanakuwa wa baba yake- na pengine ndiyo maana huyo baba anataka watoto wabatizwe katika dhehebu lake, kwani anajua pengine wengine watakuwa wake, huyo binti ana siri iliyofungwa kati yake na baba yake!
Jamaa yako aangalie pengine hata hiyo mimba si yake.
angekuwa mdogo wangu ningemwambia a-retreat! hapo kuna ushirikina. Mabinti wa siku hizi huo ujinga hawakubaliani nao. Kwanza it is not Biblical.
Hii ni kali na nzito! Hivi huyo baba mkwe anauhakika gani wa kuishi na kuona hao wajukuu anaong'ang'ania? Ikitokea Mungu amemchukua (God forbid) ataweza kufurahia chochote anachopanga? Kwa nini kuwaingiza malaika hao (watoto) kwenye mikataba wasioijua?
Binafsi nashauri jamaa awe na msimamo na akatae hilo ombi la baba mkwe mapema. Napata wasiwasi akilegea mwanzoni, yatakuja maombi mengine ambayo huenda yakawa magumu zaidi! Msimamo wake utampa heshima hata kwao kuwa kijana wao atakua baba imara kwenye familia na si legelege.
Kitendo cha kumtisha mshenga pia ni cha kuangaliwa. KiAfrika mshenga ni mtu anayeheshimika na ni kiungo muhimu hata baada ya ndoa. Kama kiungo hicho kinaanza kukosa kupewa umuhimu wake upande mmoja kitakosa maana. Jambo hilo litakua hatari kwa ndoa yenu pia.
Mwisho nashauri huyu ndugu amuombe Mungu amtie nguvu kwani jambo hili ni zito hasa ukizingatia mapenzi aliyonayo kwa mchumba wake na hali ya mchumba wake. Huyu baba mkwe ambaye hata mshenga hamuheshimu anaweza kuwa tatizo baadae katika kusuluhisha matatizo ya ndoa ambayo ni kawaida kwa kila ndoa kuwepo