Nataka kununua kiwanja Cha kijana ambaye amefariki, yaani hakuwa na mke, Wala mtoto. Wazazi wake wameshafariki. Ana ndugu zake wawili waliozaliwa pamoja
Baada ya ndugu huyo kufariki kulitakiwa kufanyika masuala yafuatayo:
1. Baada ya msiba kulitakiwa kukaliwa kikao cha ukoo ambapo kikao hicho ndio kitaangalia kama kuna wosia ama lah!
2. Kama kuna wosia basi itaangaliwa umeelekeza nini, lakini kama hakukua na wosia basi kikao cha ukoo kitachagua msimamizi/wasiamamizi wa mirathi.
3. Baada ya uchaguzi huo ambapo utafanyika sambamba na kuandaa mhutasari wa yaliyofanyika katika kikao hicho ndipo inafuata hatua hii
4. Aliyechaguliwa kuwa msimamizi ataenda mahakamani kwa ajili ya kufungua mirathi na kuomba kuteuliwa kuwa msimamizi.
5. Mahakama ikimteua na kumpa barua ya usimamizi wa mirathi ya marehemu huyo sasa ndio anakua na mamlaka juu ya kugawanya mirathi hiyo kwa wanufaika na huyo sasa ndio ana nguvu ya kuweza kuuza mali ya marehemu.
Kazi kwako mkuu. Lakini ushauri ni kuwa kama utanunua kiwanja husika usiache kufanya manunuzi hayo kwa kupitia wakili.