Ushauri unahitajika...!

Fundifundisho

Member
Joined
Jan 11, 2011
Posts
77
Reaction score
18
Kuna mfanyakazi mwenzangu anataka kumwoa binti ambaye wamedumu ktk uhusiano mwaka mmoja na nusu,
tatizo ni background ya binti huyo,.kwani kipindi jamaa anaanza uhusiano naye iligundulika kuwa binti alikuwa na uhusiano na baba yake mdogo!
Na binti alishatoa mimba mara mbili za huyohuyo baba mdogo ambaye wanaishi naye nyumbani,.jamaa alipombana binti kuhusu uvumi huo alikiri na kudai kila kitu ni kweli na kwamba alianza uhusiano na babake mdogo tangu wakiwa kidato cha pili ila kwa sasa wameachana,babake mdogo alimaliza masomo na mpaka sasa anaishi hapo hapo nyumban.,kwa kuwa jamaa anampenda msichana alivumilia mpaka msichana kamaliza shule na sasa binti anaonekana mtulivu na mwenye mapenzi ya dhati tofauti na awali alionekana kicheche!
Binti kwao mambo safi hivyo pamoja na kipato cha
Jamaa kuwa kidogo kidogo binti amekuwa akimjali na kumthamin,.baada ya binti kukiri yaliyotokea zamani na kuamua kuomba msamaha ameamua kubadiri tabia na kuwa mtulivu,.sasa jamaa anataka kumwoa anaomba ushauri wenu!
 
Yeye anamjua kuliko sisi wana Jf. Kama anaona anafaa kuolewa basi amuoe tu. Si anasema amebadilika?
 
hapo wala sio pakuoa kusema kweli....maana huyo baba mdogo akitaka kumbushia itakuwaje?
hapa ili amuo huyo demu bsi ni vizuri ukweli wa uhusiano wao uwe wazi ata kwa ndugu hapo sasa mambo yatakuwa shwari.
 
hapo wala sio pakuoa kusema kweli....maana huyo baba mdogo akitaka kumbushia itakuwaje?hapa ili amuo huyo demu bsi ni vizuri ukweli wa uhusiano wao uwe wazi ata kwa ndugu hapo sasa mambo yatakuwa shwari.
Kwa hiyo kila dada aliekua na boyfriend asiolewe? maana na wenyewe wanaweza kuja kumshawishi ili wakumbushie. Kasema dada has changed! so we can expect bamdogo akijileta atatimuliwa vipaswavo.
 
Kwa hiyo kila dada aliekua na boyfriend asiolewe? maana na wenyewe wanaweza kuja kumshawishi ili wakumbushie. Kasema dada has changed! so we can expect bamdogo akijileta atatimuliwa vipaswavo.

hapa stuation ni tofauti becoz ex bf hamna kitu to be ashamed abt lakini kugonoka na baba mdogo ni kitu cha aibu sana..hivi yule bba mdogo anaweza kumbana kuwa mie nitasema kwa watu kuwa nilikunani hii....na deu anaweza kumuachia

kuhusu ex bf mie bwana naamini kabisa kuwa nao wakuwaangalia kwa wingi. mie nikioa naenda na demu wangu saudi arabia akae kule 3 years ndio narudi nae bongo maana ukiendelea kaa haphapa ma ex watsea aolewa wapi huyo watutulikuwa twamla bwana
lakini akitoka huko suai adabu tele
 
Sasa habari ya binti kwao mambo safi inanafasi gani hapo?Ama tuseme mambo safi ndio moja ya sifa ya kuolewa?.....Mimi naona huyo binti si wakuoa maana kama aliweza kudance na babamdogo wake hawezi kushindwa kuja kudeal na mtoto wake mwenyewe siku moja.
 
Mwambie aachane nae hamna mwanamke hapo anazuga kwamba keshatemana na baba yake mdogo siku akikorofishana kidogo tu na mumewe lazima amtafute dingi mdogo alipo akapunguze machungu kumbuka hawara hana talaka
 
Amuoe 2 kwa sababu keshatubu na kuomba msamaha na kubadilika,kama Mungu anasamehe na kusahau makosa yetu sisi ni nani?halafu wapo hapo juu mnaosema hafai wangapi mmeshawahi kutest dna ya wapenzi wenu,hi dunia bwana mviringo unaweza ukawa hata wewe hapo juu unatoka na kaka yako au dada yako?kwa nini kuna siri duniani ili baba afiche wale wa nje au mama?issue si ba mdogo wala mdogo issue ni moyo na tabia,akimuoa ntamchangia,
 

Mi mwenyewe nimeshindwa kuwaelewa kwakweli. Hivi ikiwa kama hawa wanaotubu na kubadilika bado tunawatenga na kuwanyanyapaa, sasa tunataka watu wa aina gani ilhali hakuna aliye msafi?? Kama kakiri na kujirekebisha, apewe nafasi yake as a woman and somebody's wife bana!!
 

Acha kututania mzabzab, mi nadhani binti angeachia kwa kuogopa bamdogo asivujishe siri endapo angekuwa hajamtaarifu mchumba wake! Sasa hata kama bamdogo atajidai kutoa kisingizio cha kumsemea binti ilhali mchumba'ke mwenyewe anajua kila kitu, do you think kuna cha kuogopwa tena hapo?? It is not worth it! Btw, saafiiiii sana na msimamo wako wakwenda saud Arabia, unawambiaje wasiokuwa na mshiko wa kufanya hivo, watafute sponsorship au?
 
Aisey Mr! B care abt much advise! Huyu asema aoe, huyu asioe! Refar miluzi mingi humpoteza mbwa uelekeo! Mimi nakuachia neno 1 tu! Then itabaki kazi kwako na jamaa yako, kuna methali ya kiganda inasema "mwanamke na mwanaume waliokwisha vuliana nguo na wakakulana mapenzi yao hayatoisha incase mmojawao awe amekufa" katika kulisherehesha hilo ni kwamba hao waliokwisha ingiliana hata pakitokea gozigozi sijui bifu, talaka lakini ilimradi wako hai habari ndiyo hiyo.
 
Sijawahi kuiona Krismas isiyo na gharama. X mas lazima nyumba nzima mnyuke pamba mpya, msosi bomba na shangwe tele. Xmas imekaribia. kwangu hamna ushauri wa bure, chukua namba yangu uijaze na m pesa ndipo nikusaidie.
 
Duh hapo inabidi umuulize jamaa kama anamini kama watu wanabadilika tabia?

Hili suala la binti mambo safi wakati hana kazi, au ndio hela za baba mdogo maana isije siku akatoa penzi kwa baba mdogo familia isife njaa.......
 
Siku akimpigia simu akamwambia nipo kwa Ba'mdogo jamaa asimind tu. Si yupo kwa babake bana?
 
Sijawahi kuiona Krismas isiyo na gharama. X mas lazima nyumba nzima mnyuke pamba mpya, msosi bomba na shangwe tele. Xmas imekaribia. kwangu hamna ushauri wa bure, chukua namba yangu uijaze na m pesa ndipo nikusaidie.
huyu ndo BUJIBUJI bwana!!
 
sidhani ka utampata mtu ambae hajawahi kuwa na bf ka unataka hivo weka order kwa akina mama wajawazito
 

Kwenye mapenzi hamna ushauri! Mwambie jamaa aamue mwenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…