Ushauri: Unapochagua mtu wa kufanya nae biashara kuwa makini kuliko unavyochagua mke au mume

Ushauri: Unapochagua mtu wa kufanya nae biashara kuwa makini kuliko unavyochagua mke au mume

Makirita Amani

JF-Expert Member
Joined
Jun 6, 2012
Posts
1,915
Reaction score
3,422
Habari za leo msomaji wa AMKA MTANZANIA, karibu tena kwenye kipengele hiki cha ushauri wa changamoto zinatotuzuia kufikia mafanikio kwa kile ambacho tunafanya. Ni kweli kwamba njia ya kufikia mafanikio ina vikwazo vingi sana na usipokuwa umejiandaa vizuri ni rahisi sana kukata tamaa. Ndio maana kwenye kipengele hiki tunapeana ushauri kulingana na changamoto mbalimbali ambazo wasomaji mbalimbali wanazipitia.

Siku za hivi karibuni nimekuwa napokea sana ujumbe na simu za watu ambao wamefikia kukata tamaa hasa baada ya kufanya biashara na watu halafu watu hao wakawaingiza kwenye hasara kubwa. Sehemu kubwa ya changamoto hii inatokana na mtu kumwamini mwenzake ambaye ni ndugu au rafiki, wanafanya wote biashara halafu mtu yule anafanya uzembe na wanapata hasara au anatumia vibaya fedha na kusababisha hasara. Pia wakati mwingine mtu huyo anafiki hatua ya kumtapeli kabisa mwenzake.

Je nini cha kufanya ili kuepuka changamoto hii?

Kabla hatujaangalia ni kitu gani unaweza kufanya ili kuepuka changamoto hii kwanza tuangalie umuhimu wa kuwa na mshirika kwenye biashara. Ukweli ni kwamba biashara ni ngumu. Ni ngumu kuanza, ni ngumu kufanya na pia ni ngumu kupata mafanikio. Ndio maana kila siku biashara zinaanzishwa na baada ya muda mfupi zinakufa. Pia kuna watu ambao wanafanya biashara ile ile, kwa ukubwa ule ule kwa zaidi ya miaka kumi sasa.

Moja ya njia ambayo unaweza kutumia kupunguza ugumu huu wa biashara ni kuwa na mtu ambaye utashirikiana nae kwenye biashara. Mtu huyu anakuja kama mshirika na hivyo mnashirikiana kuanza au kukuz abiashara yenu. Kwenye kuanza mnaweza kuchangia mtaji, kitu ambacho ingekuwa changamoto kwa mtu mmoja, kuongeza mawazo na hata kuboresha zaidi mawazo maana vichwa viwili ni bora kuliko kichwa kimoja. Kwa vyovyote vile ushirikiano kwenye biashara ni wa muhimu sana.

Pamoja na umuhimu huu wa ushirikiano kwenye biashara na faida ambayo mshirika anaileta, mtu huyu pia analeta matatizo yake. Ndio kila mtu ana matatizo yake, hivyo atakuja akiwa kama msaada kwenye biashara , ila pia matatizo yake au mapungufu yake atakuja nayo pia. Na hapa ndio changamoto zote za biashara za kushirikiana zinapoanzia.
Nini cha kufanya?

Ili kuepuka changamoto hii inabidi uwe makini sana wakati unaamua ni mtu gani utafanya nae biashara. Ni lazima umjue kwa undani na uone kama anafaa kweli kwenda na wewe mpaka ale mtakapofikia mafanikio kwenye biashara hiyo. Naweza kusema inabidi uwe makini kuliko hata unavyochagua mume au mke.

Hii ni kwa sababu mume au mke unaweza kumchagua kwa hisia za mapenzi, amekupenda umempenda mnaoana, hata pale inapotokea changamoto mapenzi yanaweza kuwafanya muishinde changamoto ile. Ila kwenye biashara hisia inabidi zikae pembeni kabisa, hata kama mnapendana kiasi gani, kupendana kwenu hakuwezi kuokoa biashara inayokufa, mtu akifanya makosa mnapata hasara na biashara ndio imekufa.

Ili kupata mtu makini wa kufanya nae biashara fanya mambo haya matatu;

1. Mchunguze na mjue vizuri mtu unayekwenda kufanya nae biashara. Hata kama mtu unayekwenda kufanya nae biashara ni ndugu au rafiki, una kazi kubwa sana ya kumjua vizuri. Unahitaji kupata muda wa kumchunguza na kujua tabia za mtu unayetaka kushirikiana nae kwenye biashara. Jua mtazamo wake kwenye maisha ukoje, jua anaamini nini na jua mipango yake ya mbeleni ikoje.

Angalia vitu hivi kama vinaendana na vile ambavyo unavyo wewe. Kama wewe unafikiria baada ya miaka kumi biashara unayofanya iwe imesambaa dunia nzima, na mwenzako anafikiria biashara mnayofanya impatie tu fedha ya kula na kuendesha maisha umeshapotea.

Pia wakati unamchunguza mshirika wako huyo hakikisha ana sifa hizi tatu;

1. anapenda kufanya kazi kwa bidii na maarifa, 2. ni mwaminifu, 3. ni mwadilifu.

Kama amekosa hata sifa moja tu kati ha hizo tatu kimbia haraka sana, atakuingiza kwenye matatizo makubwa.

Kujua vizuri kuhusu sifa hizi tatu soma hapa; Misingi mitatu muhimu ya kujijengea mwaka 2015.
Usijidanganye kwamba mtu mzima unayekutana naye kwa ajili ya kufanya biashara atabadilika kwa sababu yako, hata akikuahidi hivyon ni uongo.

2. Yajue mapungufu yako na tafuta mtu ambaye anaweza kuyafunika.
Huwezi kufanya kila kitu, japokuwa biashara inakutaka ufanye kila kitu, kuanzia kupanga wazo zuri la biashara, kununua, kuuza, kufanya mahesabu, kutangaza na vingine vingi. Kuna baadhi ya maeneo ya biashara ambapo unaweza kuwa hafifu sana. Hakikisha mtu unayeshirikiana nae kwenye biashara yuko vizuri kwenye maeneo hayo.

Hii itawafanya muweze kufikia mafanikio kwa kukusanya nguvu zenu. Ila kama wote mna mapungufu yanayofanana mnajiandaa kushindwa kwenye biashara hiyo. Kama wewe ni mtekelezaji mzuri ila sio mbunifu mzuri wa mawazo tafuta mtu ambaye ni mbunifu mzuri wa mawazo. Ukitafuta mtekelezaji mzuri kama wewe mtatekeleza nini?

3. Wekeni makubaliano kabla ya kuingia kwenye biashara. Watu wengi wanaingia kwenye biashara kienyeji sana. Kwa sababu tu mnajuana mnaona hakuna tatizo, tunaaminiana tufanye biashara, kosa kubwa sana. Ni vyema mkakaa chini na kuwekeana makubaliano nyie wenyewe kwa wenyewe ni jinsi gani mnakwenda kuendesha biashara yenu na ni maamuzi gani ambayo hayawezi kufanyika na mtu mmoja.

Lazima muwekeane mipaka na kila mtu aheshimu makubaliano hayo. Hii itawazuia kuingia kwenye hasara. Kwa mfano mwenzako anakutana na kitu kizuri kinachohusiana na biashara yenu kinauzwa kwa bei rahisi, anaamua kununua halafu anaishia kutapeliwa. Kama mngekuwa mmewekeana utaratibu wa kwamba mtu hawezi kufanya manunuzi makubwa bila ya kumshirikisha mwenzake hasara kama hii mngeiokoa.

Haya ni mambo matatu muhimu sana unayotakiwa kufanya kabla ya kuingia kwenye ushirikiano wa kibiashara na mtu. Hata kama tayari upo kwenye ushirikiano huu na unaona kila siku unakusumbua, fanya hatua hizi tatu na muhimu sana fanya hatua ya tatu. Kaa chini na mwenzako kisha wekeni utaratibu ambao utakuwa na faida kwenye biashara yenu.

Kama utaogopa au kuona aibu kumwambia mwenzako muweke mipango upya, subiri siku utakayopata hasara na biashara kufa ndio aibu itakuisha, maana hakutakuwa tena na biashara na hata ikiwepo utakuwa umeshachoka.
Nakutakia kila la kheri katika mafanikio ya biashara yako.

TUPO PAMOJA,

Makirita Amani,

makirita@kisimachamaarifa.co.tz
 
asante, pana mpuuzi mmj ananileta usumbufu kw sabb ya ulimbukeni wke. yaani hovyo, na mkuu umeniupdate
 
Asante sana mkuu, haya mambo ndo yameniangusha mwaka jana! anyway nshaamuka nimejifuta mavumbi nasonga mbele naamini kikaango cha kupika mafanikio nichamoto sana ila ukizishinda changamoto nafanikio yanajisogeza yenyewe malangoni.
 
Last edited by a moderator:
hilo linaeleweka mkuu! ila asante sana kwa kutukumbusha na kutusisitizia..kabla watu hawajaingia ktk maumivu hayo
 
Kim nana
Ahsante kwa kuniita kwenye hii mada! Nikipata fursa, nitakuja kuchangia vipengele vingine lakini kwa sasa nataka kuchangia kipengele kimoja tu, nacho ni:"
Naweza kusema inabidi uwe makini kuliko hata unavyochagua mume au mke.
Kwanza niseme kwamba, nakubaliana na utangulizi wake kwenye hoja hii kwamba, unapochagua mshirika katika biashara basi unatakiwa kuwa makini sana... ni kweli, moja ya mambo ambayo yanafanya biashara zisifike mbali ni wrong choice ya mshirika! Hata hivyo, naomba nitofautiane nae pale anaposema unapochagua mshirika wa biashara basi unatakiwa kuwa makini kuliko unavyochagua mke na mume! Kwangu mimi, hii inapaswa kuwa conditional... nini unakipa uzito; mke/mume au biashara! Ikiwa unaipa uzito biashara kuliko mke au mume, basi mtoa mada atakuwa sahihi lakini ikiwa suala la mke au mume unalipa uzito ule ule sawa na biashara basi umakini unaotakiwa kufanyika katika kuchagua mshirika katika biashara ndio umakini ule ule unaotakiwa kufanyika katika kuchagua mke au mume coz' mke au mume wako ana direct effect kwenye biashara zako na kwa maana hiyo na washirika wako! Ukishakuwa na mke au mume asiyemwelewa mshirika wako kwavile tu hukufanya jitihada zakutosha kutafuta mke au mume atakayekuelewa kwenye shughuli zako, basi kuna hatari kwamba kimoja wapo kati ya hivyo kitapwaya... ama mahusiano ya kindoa au kibiashara! I hate to say this, in most cases, hata kama unachokipa uzito ni biashara kiasi cha kukufanya uwe makini zaidi katika kutafua mshirika kuliko mwenza, bado katika mazingira kama hayo utakuwa affected zaidi kibiashara kuliko kimahusiano ingawaje unachokipa uzito ni biashara... WHY? Ni washirika wachache sana watakaokuwa tayari kuona ndoa yako inavurugika huku chanzo cha mvurugano huo ni wewe mshirika wa biashara kwa mwenza wako... kuna hatari mshirika aka-opt kujitoa ili asionekane ndie chanzo cha kuvurugika kwenye ndoa yenu... Katika hali ya kawaida, hakuna mwenye ujasiri wa kukubali kuwa ndie chanzo chanzo cha vurugu kwenye ndoa!

Niishie tu kusema kwamba, jamii huwa inamtazama kwa jicho baya mtu anayedhaniwa kuharibu ndoa ya mtu mwingine kwa sababu yoyote ile kuliko anavyoangaliwa mtu anayedhaniwa kuharibu uhusiano wa kibiashara wa watu wengine... kutokana na hilo ndio maana nikasema kuna hatari mshirika aka-opt kujitoa endapo hukutumia umakini ule ule wa kuchagua mwenza anayekuelewa!
Kim nana, kwa sasa, niishie hapa, lakini Inshallah, nikipata wasaha nitakuja kwenye vipengele vingine!
 
Asante kwa nondo chige kumbe sijakosea kukuita, haya tunasubiri nondo nyingine...
 
Last edited by a moderator:
Naogopa sana tena sana na sana kufanya biashara tena. Hasa na mswahili. Nilitapeliwa laki nne 2008 narafik Ninayemuamin na ijatoka moyon kitu nitamfanyizia wewe ngoja tu. All in all si kila mtu anaweza biashara i believe in hard work and savings
 
Naogopa sana tena sana na sana kufanya biashara tena. Hasa na mswahili. Nilitapeliwa laki nne 2008 narafik Ninayemuamin na ijatoka moyon kitu nitamfanyizia wewe ngoja tu. All in all si kila mtu anaweza biashara i believe in hard work and savings

Samehe na u-move on mkuu. Kwa kuendelea kushikilia hilo unaumia wewe zaidi ya anavyoumia yey.
Tumia ulichojifunza kutokurudia tena makosa.
Usiogope biashara kwa sababu ya hasara uliyopata.
Watu wanapata ajali kila siku na bado wanapanda magari...
 
Asante sana mkuu, haya mambo ndo yameniangusha mwaka jana! anyway nshaamuka nimejifuta mavumbi nasonga mbele naamini kikaango cha kupika mafanikio nichamoto sana ila ukizishinda changamoto nafanikio yanajisogeza yenyewe malangoni.

Ni kweli mkuu safari ya mafanikio sio rahisi kama wengi wanavyoamini.
Hongera sana ma nakutakia kila la kheri.
 
Mkuu umenikuna penyewe hasa mwaka jana nilikuwa na mtu kama huyo hakuwa na focus yoyote nimeachana naye sasa nimeanza mwaka mpya peke yangu nione nitaumaliza vipi
 
biashara kitu cha ajabu sana mm saizi nilisha kata tamaa kabisa kwasabu mtu ambae unamuamini ndio anakuingiza mjini na watu siku hizi ni watu wa plan sana unakuta anakuambia mara mzigo umepotea mara sijui nimeibiwa wakati si kweli
 
Naogopa sana tena sana na sana kufanya biashara tena. Hasa na mswahili. Nilitapeliwa laki nne 2008 narafik Ninayemuamin na ijatoka moyon kitu nitamfanyizia wewe ngoja tu. All in all si kila mtu anaweza biashara i believe in hard work and savings

Pole sana mkuu, yaani kwenye biashara kuna udanganyifu wa kila aina
Biashara inakutaka sometimes uwe dikteta na moyo mgumu kadhalika ku reason mambo kwa wakati
 
Biashara yoyote ina challenge zake na kama unataka kufanikiwa kibiashara mi Naona unatafuta mtu mwenye kujua zaidi hiyo biashara kama unataka kuwekeza asilimia kubwa katika biashara ili wewe uwe msemaji wa mwisho katika maamuzi. Haijalishi uwe unamjua kiasi kikubwa hivyo maadam anawekeza pia % fulani. Kwa tz sio ngumu ila ni kuandikishana tu mkataba na kila wakati kupigiana mahesabu yanaendaje na malipo yote yawe bank kwenye joint account. Sijui ni biashara inazungumziwa lakini cha muhimu ni kufuata taratibu zote za kibiashara lakini kama utafanya bila mipangilio mizuri ni lazima utapeliwe. Mimi nimefanya biashara nyingi na partners na zingine nimeingiza pesa tu nikiwa kama sleeping partner na kazi zinaenda. Utapeli unakuja unapomshirikisha mtu asiejua anafanya nini na alikuwa anafanya nini mwanzo. Labda nimeeleweka hapo
 
Back
Top Bottom