Emmanuel S Jonathan,
Kwa Tanzania, spare parts za Honda, Hyundai, Mazda upatikaji wake ni mgumu na hata ukizipata gharama yake ni kubwa. Nachokipenda ni kuwa spare zake bado mchina hajatia mkono wake,hivyo ukizipata na kuziweka ktk gari yako zinadumu kwa muda mrefu sana.
Honda accord zipo za aina tatu tofauti
1. Honda Accord
2. Honda Coup
3. Honda Wagon.
Mfano ukitaka kuagiza 2003 HONDA ACCORD toka Japan.
Transmiss ni automatic
Engine Size yake ni 2,350cc
Jumla ya seats ni 5
Milango ni 4
Mafuta ni Petrol
Kama utainunua toka Japan, gharama ya chini kabisa ya kuinunua
2003 HONDA ACCORD ni CIF= $2,475 (zipo zenye bei Zaidi ya hapo,nimekupa bei ya chini kabisaaaaa).
Llakini ukumbuke pia kuwa inabidi utoe gharama ya I=insurance ambayo kwa sasa na kwa sheria mpya inatakiwa kulipiwa Tanzania.
Kwa maana hiyo basi bila "I" bei itakuwa ni C&F=$2,399 hapo ni mpaka inafika bandarini.
Kwa ninavyoona kuhusu Engine size (2,350cc) yake,sio mbaya sana ktk Matumuzi ya mafuta,lakini ni lazima ujipange.
Ni nzuri kwa safari ndefu haichoshi.