Ushauri: Uwanja wa Gwambina Complex ufungiwe,Pitch ni mbovu

Ushauri: Uwanja wa Gwambina Complex ufungiwe,Pitch ni mbovu

Abby Newton

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2017
Posts
1,252
Reaction score
2,253
Natazama mechi ya ligi kuu kati ya Gwambina vs Jk Tanzania. Kwakweli huu uwanja wa Gwambina Complex Pitch imechoka na ni dhahiri uwanja umekosa hadhi ya kutumiwa kwa michezo ya ligi kuu kwa sasa. Pitch ina vinundu vya manyasi na vipara vingi, hali inayosababisha mpira wa chini kushindwa kuchezeka. Ni mwendo wa butua butua tu.

Kwa hadhi ya ligi yetu viwanja kama hivi vinatutia aibu. Nashauri kamati ya ligi ichukue hatua iufungie mara moja hadi hapo watakapofanya marekebisho.

Over!
 
Ni wapi imeandikwa kuwa mpira wa miguu lazima uchezwe chinichini. Wakataze basi kitumia vichwa.
 
Ni wapi imeandikwa kuwa mpira wa miguu lazima uchezwe chinichini. Wakataze basi kitumia vichwa.
We jamaa mbona una hasira sana timu yako Utopolo nini?[emoji12][emoji12]
 
We jamaa mbona una hasira sana timu yako Utopolo nini?[emoji12][emoji12]
We koma! Nani ashabikie maji taka? Wao utopolo ndio wanaona viwanja vibovu wakati wenzio walicheza hapo na kushinda.
 
Back
Top Bottom