Tunajenga ofisi ya kikundi chetu na tunahitaji kuweka vigae kwenye sakafu.
Hapa kwetu udongo ni mwekundu ambao ukipata maji unakuwa tope na unateleza sana. Naomba ushauri wa vigae vya sakafu vinavyofaa kwa kuzingatia:
- Kampuni na nchi vilikotengenezwa.
- Rangi inayofaa.
- Kipimo bora, fano 40x40, 50x50 nk.
- Sura yake, mtelezo, mng'ao nk.
- Na mengine kwa kuzingatia utaalamu.
MAMBO YA KUZINGATIA KABLA
HUJANUNUA VIGAE (TILES)
1. Matumizi ya eneo husika - Sehemu zenye majimaji hazihitaji vigae vinavyoteleza (ungrazed) mfano chooni, bafuni, na jikoni ukilinganisha na sehemu ambazo hakuna matumizi makubwa ya maji mfano sebuleni, sehemu ya kulia chakula na vyumba vya kulala.
2. Upatikanaji - kwa kawaida inaweza kuwa aina ya kigae unachotaka ukawa uliangalia kwenye mtandao na ukakipenda lakini kumbe bado katika mazingira yako haijafika basi ni vyemba kutafuta aina nyingine illyopo karibu na wewe au kufanya mchakato wa kuiagiza.
3. Uwezo wake na muda wa kuaribika - vigae vinatofautiana uwezo na muda wa kuaribika kutokana na malighafi/material iliyotengeneza hivyo ni vizuri kuchagua vile vinavyokaa muda mrefu ili usipate shida ya kurekebisha/maintenance mara kwa mara.
4. Gharama (mfuko wako) - ukiachana na sababu zilizoelezewa hapo juu, pia ni lazima uangalie na bei ya vigae hivyo ili uweze kufanya upembuzi yakinifu kulingana na kiwango cha fedha ulichonacho, usijiumize sana kwa sababu ya weza kuwa vipo vingine vyenye bei angalau na vinafanana na hicho unachotaka.
KARIBU UPATE ELIMU BURE KUHUSU UJENZI WA TILES
[emoji3513] +255 714 122 011
[emoji536] Tupo Goba Dar es salaam
[emoji593] Popote tunakufikia [emoji1139][emoji1254][emoji1268][emoji1060][emoji1156]
#NyumbaYakoFahariYako
#IfanyelweYaTofauti
#TupeTuipandisheThamani #jenganasi