Ushauri: Vigezo vya kuzingatiwa na mamlaka ya uteuzi wa Wakurugenzi Watendaji

Ushauri: Vigezo vya kuzingatiwa na mamlaka ya uteuzi wa Wakurugenzi Watendaji

Koryo2

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2016
Posts
2,056
Reaction score
2,519
Mkurugenzi Mtendaji wa Jiji, Manispaa, Miji na Halmashauri ni nguzo muhimu sana katika kubuni, kusimamia na kutekeleza majukumu yote ya eneo analosimamia. Mkurugenzi Mtendaji awe ni mtu aliyebobea katika masomo yake, ujuzi na kwa kweli ni mtu ambaye anapaswa kuwa amekulia katika Halmashauri au Utumishi wa Umma.

Uteuzi wa Wakurugenzi Watendaji katika Awamu ya Tano ulikuwa na kasoro kubwa sana. Wengi wao waliteuliwa kwa upendeleo, baadhi hawakuwa na sifa ya kuwa Wakurugenzi, wengine walioteuliwa ni wale walioshindwa kwenye kura za maoni ya CCM bila kuwa na uelewa na Halmashauri, wengine walikuwa viongozi Kanisani nk.

Hivyo naishauri Mamlaka ya uteuzi awamu hii wasifanye makosa kama ya awamu ya tano kuhusu uteuzi wa Wakurugenzi Watendaji. Zifuatazo ni sifa zinazotakiwa kuangaliwa katika uteuzi:-

(1) Kuwa na kisomo siyo chini ya digrii.
(2) Kuwa na ujuzi usiopungua miaka 10 katika Utumishi wa Umma.
(3) Awe ni yule ambaye amekulia katika kufanya kazi katika Halmashauri kwa miaka angalau kumi. Tunao watumishi wazuri sana katika
Halmashauri Mfano. Waweka Hazina, Maafisa Utumishi, Waalimu, Maafisa Kilimo, Maafisa Ardhi nk.

Chonde chonde uteuzi wa awamu hii ufanyike kwa umaakini mkubwa sana Wote ni mashahidi tumeona ripoti ya CAG.
 
Jiwe aliweka wengi kwa ajili ya uchaguzi, yaani kura apate yy.

Subiri Mama anajua haya yote.

Ila sio wote wapo wazuri, ila madiwani wengine ndo wapiga deal wakubwa

Ona clip ya kikao cha baraza la Kinondoni leo... wilaya yenye risiti feki, leseni feki kila kona.

Halaf unasikia Mayor anakimbilia cover ya u CCM!

Komaa Mkurugenzi fagia wote hao wezi wa mapato ya serikali!
 
Back
Top Bottom