Ushauri: Vituo vyote vya Redio na Runinga viwe na vipindi maalum vya jinsi ya kujifukiza

Ushauri: Vituo vyote vya Redio na Runinga viwe na vipindi maalum vya jinsi ya kujifukiza

Freed Freed

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2017
Posts
6,547
Reaction score
7,167
Habari Wana wa JF.

Kutokana na ushauri mujarabu wa Rais Magufuli ambao pia umepokelewa kwa shangwe hata na wataalamu wa Afya, nashauri vituo vya Redio na Television vianzishe vipindi maalumu vikituelekeza jinsi ya kujifukiza dhidi ya Covid 19.

Hatua hii ni muhimu sana katika kipinndi hiki cha kupambana na dubwasha hili hatari. Kama kituo cha habari hakitakuwa na kipindi hiki, kishurutishwe kufanya hivyo.

Vipindi hivi viwe Mara mbili kwa siku yaani asubuhi sana na pia marudio yafanyike usiku. Hii itasaidia watu wanaokuwa bize na kazi mchana kutopitwa na elimu au maarifa haya muhimu.

Wasalaam.
 
Walianza na vipindi vya maombi dhidi ya Corona, sasa vipindi vya kupiga nyungu vitaanza na mwisho kabisa vitakuja vipindi vya maombolezo ya kitaifa baada ya Corona kulitafuna taifa.

Si bado tunadhani mzungu alikuwa mjinga aliposema Corona ni hatari.
 
Tusitishane, kufukiza ndiyo mada
 
Tusitishane, kufukiza ndiyo mada
Hakuna wakukutisha, wewe mwenyewe utakuja hapa hapa kuukiri huo ukweli.
Bado unadhani Corona ni nadharia tu huku ukiamini kuwa hizi blah blah za kujifukiza zitasaidia kitu.

Muda utakupa majibu.
 
Achaneni na huu upuuzi, kujifukiza sio tiba ya corona maana hamna majaribio yoyote waliyofanya na watu wanazidi kupukutika, kila mtu anakuambia mizizi na magome yake bila kuwa na uhakika.

Sasa hivi ilitakiwa serikali ihangaike kufuatilia dawa ambazo nchi nyingine imezitumia na kuwa na matokeo chanya.

1. Madagascar kuna tiba ya miti asili (CVO)
2. Marekani kuna dawa za kizungu Remdesivir imeonyesha matokeo chanya

Pia serikali iangalie uwezekano wa kupata ama kutumia vipimo vya gharama ndogo vinavyoanza kufanyiwa majaribio Senegal.
 
Hakuna wakukutisha, wewe mwenyewe utakuja hapa hapa kuukiri huo ukweli.
Bado unadhani Corona ni nadharia tu huku ukiamini kuwa hizi blah blah za kujifukiza zitasaidia kitu.

Muda utakupa majibu.
Bado unazidi tu kutisha na kuwaogopesha watu?
 
Back
Top Bottom