Ushauri wa Bashiru kwa Membe na maana yake

Ushauri wa Bashiru kwa Membe na maana yake

GARETHBALE

Member
Joined
Dec 22, 2013
Posts
76
Reaction score
333
Hii tuanze tu hata bila kusalimiana wala kuzingatia itifaki maana sasa kila mwananchi ana maswali mengi kuliko majibu hivyo salamu na itifaki hazisaidii kutafuta majibu ya maswali vichwani wa wananchi.

Tujiulize; Bashiru anashauri Membe ajiunge na upinzani na huko akagombee urais. Sasa kwa ushauri huu tunahitaji ushahidi gani zaidi kwamba kilichomfanya Membe afukuzwe CCM ni nia yake ya kugombea urais ndani ya CCM? Bashiru kwamaneno mengine anahalalisha alichokisema Membe kwa 100%. Anachotuambia Bashiru kwamba ukipingana na bosi wake na kutaka kugombea kiti cha bosi wake utafukuzwa.

Tujiulize pia; Bashiru anashauri Membe akate rufaa na kwamba peni Bashiru imejaa wino tayari kumruhusu arudi. Ili tujue anachotaka Bashiru tujue tujiulize swali moja la msingi: Je Membe ameulalamikia uamuzi mahala popote kwamba haukuwa wa haki? Hii washawasha ya Bashiru kumshauri Membe akate rufaa inatoka wapi? Inatokana na wasiwasi gani?

Tuendelee kujiuliza; Bashiru anashauri Membe ajiunge na upinzani na huko agombee urais. Sasa hapa inabidi utumie ubongo wa ziada kujua lengo hasa la Bashiru katika ushauri huu. Tuanze. Musiba alimtuhumu Membe kuhujumu uongozi wa juu, Membe kimya. Musiba hakuishia hapo, akapendekeza Membe afukuzwe chama, Membe kimya. Bashiru huyu huyu akajitika madafu ya Musiba na kumtaka Membe ajieleze, Membe akamtafuta Bashiru lakini Bashiru akaingia mitini akapotea Membe kimyaa.

Kisha Bashiru akasikika mara kadhaa akisema ni ruhusa mtu kuhama CCM. Kitendo cha propaganda kikatumia muda mwingi kupiga propaganda za Membe kuhamia ACT. Membe kimyaa. Mtego wa Bashiru kumtaka Membe ahame chama ukabaki ukibadirishwa chambo tu. Sasa nadhani hadi hapa tunajuwa maana ya ushauri wa Bashiru kumtaka Membe aende upinzani.

Nisimalize hapa bila kujiuliza kile ambacho Membe alihoji na waandishi wakashindwa kumhoji Bashiru jana. Membe "alikatwa" au "kupata kura chache" NEC mwaka 2015. Haki yake ya kupiga na kupigiwa kura kwa mujibu wa katiba alipewa. CCM sasa inashindwa wapi, inaogopa nini, inakosa nini, au inatatizo gani "kumpiga ngwala" tena Membe kwenye uchaguzi wa ndani CCM? Swali hili kwa undani wake katika majibu yake ndio chanzo cha mtafaruku ndani ya chama hiki kikongwe. Ni chama kinachoathirika na virusi vya korona kwa kasi ya ajabu.

Nitarudi baadaye kidogo.

By Maarifa Kupapasa-Maarifa Kutomasa.
 
Hivi, kwani yule jamaa aliyekuwa anaongea na Membe kwenye ile clip ilizagaa siku za nyuma, na ambayo imemletea Membe kufukuzwa chamani, jamaa naye wamemfukuza? Kama hawajamfukuza, kwa nini mazungumzo wafanye watu wawili lakini aadhibiwe mmoja? Au mmoja alikuwa shushushu kwa mwenzake?

Sikuwepo jukwaani siku kadhaa, hivyo sijui kama swali hili lilishaulizwa humu jukwaani.
 
Ni chama kinachoathirika na virusi vya korona kwa kasi ya ajabu.[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji134]


Jr[emoji769]
 
Membe hakukuwa na haja ya kumfukuza, maana hata asingepata kura nyingi.

Huenda angevunja rekodi ya kupata kura chache katika historia ya CCM.
 
Ile hotuba ya Waziri Zungu baada ya kiapo cha UWAZIRI, na hapa nanukuu, "mgombea pekee wa kiti cha urais uchaguzi mwaka huu ni JPJM".
Kwani alishatangazania mwingine? Nini kilimpelekea huyu Mzee kutoa kauli ile?
Lisemwalo lipo na laja pia. Bashiru acha hizo!
 
Membe hajafukuzwa,

Kilichofanyika ni kupata mgombea upande wa Upinzani..Maana kuna uwezekano Mkubwa wa Upinzani kususia Uchaguzi..Zanzibar tayari 2015,Serikali za Mitaa2019..

Ikitokea Uchaguzi Mkuu ukasusiwa na Upinzani ni hatari zaidi kwa Nchi Marafiki pamoja na zinazotupa Misaada...

Kama ulisikia clip zote,Membe, Kinana,&Makamba..ya Membe ilikua na nafuu kuliko zote.

Kama ni Kuitikia wito Membe alikua wa Kwanza lakini wengine Wakaishia nje..kwanini afukuzwe yeye?!

Membe ni Mkakati wa CCM..kama kungekuwa na hofu kiunganishi wa hawa Wawili ni Jk..

Upinzani Wawe Makini..Bila Tume Huru susieni Uchaguzi.
 
Sioni mantiki ya kumjadili Membe na ugomvi wake huko CCM na bio za urais November. Kwa CCM, JPM keshashinda second term.
Vinginevyo hata uchaguzi wenyewe kwa mazingira yalivyo kisiasa utakuwa sanaa tu!



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom