Ushauri wa biashara kwa mtaji wa 1.5ml

meezy

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2014
Posts
685
Reaction score
1,207
Mimi ni mwanafunzi wa ninaeingia second year katika chuo kimoja hapa Mwanza.Nina kama milion 1.5 nataka nijifunze biashara stil nikiwa bado nipo chuo.

Naomba ushauri wenu wadau nini nifanye na ni biashara gani itanifaa.
 
Mshika mawili moja humponyoka.hifadhi benk hizo fedha ukimaliza chuo jiajiri mwenyewe.
 
Wekeza pesa yako huku ukiwa unaendelea na masomo achana na mambo ya biashara yatakuchanganya, hadi utakapomaliza masomo yako utakuwa umeshakomaa kiakili, biashara kwa kuisikia au kumwona mtu anaifanya ni rahisi sana lakini ukijiingiza ndio utaona ugumu wa biashara.

Na ukumbuke biashara ina faida na hasara usitegemee faida tu, sasa kwa msingi wako huo unaotaka kuanzia unaweza piga mweleka na wewe ni bado mgeni kwenye biashara
 
Mimi ni mwanafunzi wa ninaeingia second year katika chuo kimoja hapa Mwanza.Nina kama milion 1.5 nataka nijifunze biashara stil nikiwa bado nipo chuo.

Naomba ushauri wenu wadau nini nifanye na ni biashara gani itanifaa.

Hongera boss una hela nyingi mno wemzako tulianza na fifty thousand! nakushaur anzisha huduma ya mpesa kulipa na kuweka hela ndondogo na kuuza vocha wateja watakufuata mpaka chumban na shule itakwenda km kawa wasikutishe ww upo chuo kikuu mkuu big up kwa kuuliza
 
ushauri mzuri wa Mpesa na kuuza vocha hapo shule ndio yenyewe hiyo utawauzia hadi ma prof, usikopeshe utapunguza wateja
 

ushauri mzuri
 
Ingekuwa enzi zetu ningekuambia nunua kamera kali ili uwe camera man maana chuoni kuna kila aina ya matukio kuanzia birthday lakini siku hizi mambo ya digital yameharibu, anyway naungana na wale waliosema uwekeze kwenye Mpesa na vocha
 
Mshika mbili moja humkimbia.......fuatilia bei ya hisa za TBL, CRDB etc. Kwa 1.5mil utapata hisa za kutosha, tulia usome. Ukihitimu tu shule kachukue hisa zako uza, utapata bonge la mtaji na utaweza kuanzisha biashara kubwa uitakayo. Hizo sijui M-pesa sijui nini, zitakuchanganya tu maana zitakula muda wako ambao ungetumia kusoma.
 
Mimi ni mwanafunzi wa ninaeingia second year katika chuo kimoja hapa Mwanza.Nina kama milion 1.5 nataka nijifunze biashara stil nikiwa bado nipo chuo.

Naomba ushauri wenu wadau nini nifanye na ni biashara gani itanifaa.
Hongera sana mkuu kwa kuwa na wazo zuri la kuanza kujifunza biashara. Lakini kwa ninavyoona watu wanavyokushauri hapa WANAKUOGOPESHA na kama ukiwasikiliza HUTAWEZA kufanya jambo lolote kwenye maisha yako.
Asikudanganye mtu kwamba eti wewe ni mwanafunzi hivyo ukifanya biashara utafeli, wazembe ndio wanaofeli ila kama wewe sio mzembe utapata mafanikio makubwa sana. Wanakuambia usubiri mpaka umalize, hivi hawawaoni wenzako wanaosota mtaani bila ajira? Wanakushauri ukanunue hisa hivi unaelimu ya hisa hata kidogo? Je hawajui kufuatilia hisa zako na soko la hisa kwa ujumla ni kazi kubwa zaidi? Maana uchumi wa sasa ni very fragile anyatime thamani ya hisa inaweza kushuka na ukawa out of business soon. Ni bora ukafanya biashara yako mwenyewe na kama utashindwa utakuwa umejifunza somo muhimu la mafanikio, maana hutorudia kosa tena.
Naomba nimalizie kwa kukupa mpango rahisi;
Siku yako ina masaa 24, toa masaa 8 ya kulala. toa masaa nane ya kuhudhuria masomo darasani, unabaki na masaa nane kwa siku.
Hayo masaa nane toa masaa manne ya kujisomea mambo yako ya shule(masaa manne kweli na kwenye muda huo hakuna kuchat wala kuingia kwenye mtandao), unabaki na masaa manne. Sasa amua haya masaa manne unayatumiaje. Wanafunzi wengi wa vyuo wanatumia masaa haya kuzurura, kuangalia muvi(series ndio usiseme) kushindwa kwenye mitandao ya kijamii na vitu vingine ambavyo havina msaada kwako. Ila kwa kuwa tayari wewe uko smart tumia muda huu kusimamia biashara utakayoanzisha, unaweza fungua biashara yoyote kulingana na mazingira ya hapo chuoni. Kikubwa ni ile nia ya dhati ya kufanya biashara na kuwa na malengo. Pia usipoteze hata sekunde ya muda wako kufanya jambo ambalo halina msaada kwako. Kuhusu kupumzika, unapumzika unapolala.
Nakupongeza sana mkuu na nakushauri songa mbele usisikilize wanaokukatisha tamaa.
Kama utahitaji ushauri zaidi unaweza kuwasiliana na mimi kwa email amakirita@gmail.com au simu 0717396253. Karibu sana.
 
Mkuu ntakutafuta na mi ni mwanafunzi nipo dar hili suala limekuwa likinitesa sanaa. Nahitaji kuwa na chanzo cha kuniingizia hata pesa ndogo ndogo tu ili mradi ziwe zangu na kwa njia halali
 
Nimejifunza kitu hapa!
 

Mawazo hasi kabisa haya, sijui mnayatoa wapi. Sisi watoto wa maskini tunazijua shida, nyie watoto wa mama chuoni ni kuangalia muvi, kuchat na kutongozana tu mkitumiwa home allowance ni kukesha bar! Nakupa mfano, mimi nimejisomesha mimi sijakopa pesa wala kutumiwa pesa na mzazi, nilivomaliza f6 nikajichanganya mtaa mtaa kutafuta kianzio, nimepiga kitabu huku nakomaa na biashara, niko mwaka wa pili nasomesha mdogo wangu mwaka wa kwanza na mtoto wa dada yangu Olevel, weekend naenda kukaa golini nasanya au naendesha, jumatatu asubuhi narejea chuo!
 
Swala la kupata loss kwa age yang pia ni sehemu ya kujifunza maisha..na swala la kusahau masomo uko ni kutojielewa..nmeomba ushaur nijfunze biashara m2 ananshaur hisa,kwa umri wang hisa bado san..lengo lang ni kujifunza maisha..nashkuru kwa wte mlionpa ushauri uzur
 
Mkuu ntakutafuta na mi ni mwanafunzi nipo dar hili suala limekuwa likinitesa sanaa. Nahitaji kuwa na chanzo cha kuniingizia hata pesa ndogo ndogo tu ili mradi ziwe zangu na kwa njia halali

Karibu sana mkuu. Unaweza pia kutembelea AMKA MTANZANIA www.amkamtanzania.com na kujifunza mengi yatakayokuamsha na kukuhamasisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…