Ushauri wa Biashara ya kuwekeza, kwa Tsh 2 million (Mwanza)

Tafuta kijiwe maeneo ya stand/penye msongamano wa watu,anza kuuza kahawa,chai ya tangawizi,kashata n.k
 
ha ha ha tatizo watu wanapenda kusikia biashara nzuri nzuri kama za kuuza magari n.k wakati mtaji auruhusu
hapo ndo mamotivation people wanapotuweza....yaani wanakudanganya eti sio lazima uanze na kikuabwa unaweza ukaanza na kidogo zen utafikia malengo ya kupata kikubwa kwangu mimi nasemaga huo ni upuuzi tu maisha hayana fomula sio lazima uteseke ndio ufikie mafanikio...........mi nilishajiwekea msimamo siwez anza kujiajiri bila kuwa na 30m cash ukiachilia mbali pesa ya kujikimu nikishindwa hapo basi ni bora kuendelea kuajiriwa tu hakuna namna
 
Nenda kaanzishe salon ya kiume ''a very classic barbershop'' pale rock city mall then baada ya miezi sita urudi hapa kunishukuru, huwa napata shida sana sehemu nzuri yakujiweka sawa nikiwa mwanza
Wewe huijui Mwanza vizuri...Barber shop classic zipo kibao tu hapo mitaa ya rufiji mpk dampo huko...afu rocky city mall unajua gharama ya pale kweli!??
 
Fungua butcher ya nyama na samaki kwa pesa hiyo inatosha sana.
 
Nunua boda boda
Wakuu, nnaomba ushauri na mawazo juu ya biashara nzuri ambayo naweza kifanya Jijini mwanza, nikiwa na kiasi cha Tsh 2 million. Nahitaji kwenda kuishi na kufanya Biashara mkoa huo, Ushauri, Maoni au Mawazo utakua msaada kwangu.
Ahsante.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…