alongakeke
Member
- Feb 3, 2017
- 98
- 30
wakuu habar zenu. Mimi nilikua mfanyakazi wa kampuni flani ya uchimbaji migodini . Mimi ni mkazi wa Mwanza.Niliacha kazi na kuanza kufatilia mafao yangu NssF na hatimaye baada ya mwaka mmja nimelipwa mafao yangu yote . Nna mtaji uko tayar Tsh 210m cash na Nna mpango wa kufanya ujasiriamali lakn nna kwama nijikite kwenye biashara gan maana kila anaenishaur ananiambia biashara zile zile zilizozoeleka tena maeneo yale yale.mmoja jana kanishaur biashara ya nguo kufata dubai, mwingine alinipa idea ya kufungua bar mkoani mwanza,mwingine kanishaur ninunue hiace tano niziweke ruti ya igoma buhongwa au airport buhongwa, mwingine kaniambia nianzishe shule, wakuu napata tabu maana naona kama biashara hizo ntakua nafanya kitu kile kile kwa namna ile ile hivyo itakua ngumu kujitofautisha na wengine hata ROI itakua ndogo sana na itachukua muda sana, Naomba wakuu ushauri na mwenye idea ya biashara yenye ubunifu na utofauti kidogo anisaidie naweza hata ku fund idea yako tukafanya patnership. Niko tayar kufanya Bbiashara mkoa wowote wa tanzania sio lazima Iwe Mwanza tu.