Ushauri wa Bure: Diamond saidia baba yako

Nyadundwe

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2008
Posts
227
Reaction score
260
Naandika nikiamini kwa namna moja au nyingine ushauri huu utamfikia huyu kijana Diamond. Yeyote asiye na maelewano na wazazi/mzazi wake pia inamuhusu. Na wazazi wanaotelekeza vizazi vyao pia wanaweza kujifunza jambo.

Mimi ni mmoja kati ya watu wanaopenda namna Diamond anavyojituma katika kazi pamoja na ubunifu katika muziki na biashara ya muziki. Pia amekuwa mstari wa mbele kusaidia vijana wenzake, hususan waliotoka katika hali duni kimaisha kama ilivyokuwa kwake, kupata maendeleo kupitia sanaa. Tumeshuhudia hali kadhalika mara kadhaa akirudi maskani Tandale na kuwasaidia wakazi wa huko, kidogo alicho jaaliwa, na mengine mengi mazuri.

Yapo pia mambo kadhaa ambayo sifurahishwi nayo kuhusu yeye, lakini nitalizungumzia hili la kumtelekeza Baba yake. Nimeona mahojiano ambayo baba Diamond amefanya na online TV moja. Ni wazi kwamba huyu mzee alitibuana na demu wake Sandra - mama Diamond, akatimka nyumbani na kutelekeza familia. Anasema wakati huo Diamond alikuwa na akili yake nzuri tu, hivyo huenda Diamond aliathirika sana kisaikolojia kwa Baba yake kutokomea kusikojulikana na kuwaacha yeye na mama yake hawana hata unga robo.

Kutokana na maelezo yake aliyotoa na mazingira ya nyumbani kwake, huyu mzee ana hali ngumu. Baba Diamond sasa hivi anafanya biashara ya kukopa viatu vya mtumba Ilala, anarudi kwake magomeni anaviosha na kung'arisha kisha anatembeza mtaani, yaani Mmachinga typical. Anapoumwa kwa mfano, anakuwa hana hata fedha ya matibabu, hivyo kugeuka ombaomba. Kutokana na maelezo ya Mzee mwenyewe, majirani na mdogo wake Diamond anayeishi na baba yake, Diamond kufika kwa mzee wake ni tokea yuko na Wema!

Kilichonifanya kuandika huu uzi ni kwamba Baba Diamond ameomba msamaha kwa makosa aliyoyafanya. Tena amesema kwa uchungu kabisa, kwamba hata Mwenyezi Mungu husamehe. Kwa nini , yeye asisamehewe?. Binafsi naona imefika wakati Diamond akunjue moyo wake na kumsaidia Baba yake. Katika Qur'an, ipo wazi kabisa, kwamba baada ya Mwenyezi Mungu, wanafuata wazazi. "Be grateful to Me and to your parents; to Me is the [final] destination." (Quran 31:14). Mzee Abdul alikosea kumtelekeza mtoto Diamond, haijalishi walitibuana nini na mama Diamond. Diamond hajui nini hasa kilitokea. Mzee ameomba msamaha, anapaswa kusamehewa na maisha yaendelee.

Diamond rudisha maelewano na umsaidie baba yako. Amejutia na ameomba msamaha. Kwa sasa haikupunguzii chochote kumsaidia mzee wako aishi maisha ya kawaida, ya angalau ajue familia yake itakula nini jioni. Utakuwa na amani, Itakuongezea heshima katika jamii, na zaidi utapata credit kwenye daftari lako la Akhera. Maisha yenyewe ndiyo haya. Ukiishi sana 80. Ukiishi zaidi ya 80 ni maumivu tu, uwe na hela au huna. Akifa huyu mzee katika hali hii, Diamond utaaibika Duniani na akhera.
 
Nimeona YouTube mzazi ana busara sana kaongea mengi huku akimtakia mafanikio na nyota ing'are. Kasema suala la kumwalika harusini ni lake yeye Diamond cha msingi anapenda aone diamond anaoa na sio kugeuza nyumba daguro!!. Sijawahi kununua kazi ya Diamond na sio shabiki wa miziki yote ya Tz isipokuwa miziki ya OTTU JAZ BAND. Kijana nimemdharau sana kwani sisi wakristu tunafundishwa samehe saba mara sabini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ng'wanapagi,
Hujajua maumivu ya kukataliwa na mzazi wewe tena hilo neno la kumdharau futa.
Ni maumivu yasiyoelezeka wewe unazungumza tu kwa sababu ulipata malezi ya wazzi wote.

Kupewa pesa si tatizo yule mzee pesa anapata, tatizo ni msamaha ni kitu kigumu sana mwanadamu kukitoa, haihitaji media ili kupata msamaha anahitaji wasuluhishi shauri yake.
 
Unajuaje kama na mimi nimelelewa na mama na bado nikamtafuta baba nikiwa mtu mzima. Nimesema na ninarudia tena dini yangu inasema samehe saba mara sabini

Sent using Jamii Forums mobile app
Narudia tena Msamaha wa mwanadamu kwa mtu aliyemkosea ni mgumu sana kutolewa.

Siku hizi kuna misamaha mingi ya kinafki kama "Basi nimekusamehe" si kweli amini usiamini 7×70 iliisha 15 century.
 
Mnamuonea tu Huyo diamond ..... (mimi huwa sivutiwi na Tabia zake chafu chafu) ambazo zimenifanya nisimpende kabisaa"

Lakini kama ni kweli baba yake Alimtelekeza alipo kuwa mdogo kwaajili ya mgogoro na mzazi mwenzie

Basi ana stahiki kupatwa na hicho kinacho mfika " kwa sababu mtoto hakuwa na makosa

Huwa tuna vuna tunacho kipanda' so suala la kumuona diamond kuwa hamtendei haki baba yake " wakati baba yake mwenyewe mbegu aliyoipanda ndio hiyo" ni wazi mtakuwa mnanuonea tu diamond"....., mlitaka mzee avune karanga baada ya kupanda kokoto .. !?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu endelea kumsapoti msanii wenu mie band yangu OTTU JAZZ ishajifia

Sent using Jamii Forums mobile app
Sawa sawa, mtafute Dina Marios wa EFM atakueleza anakutana na hizi kesi mno yeye mwenyewe ni shuhuda kupata msamaha kwa mzazi wa namna hii ya Mzee Abdul ni ndoto bila kujali jinsia ya mzazi.

Pesa atapata ila hazitamsaidia lolote msamaha kwanza
 
Wakati ukijitwika utakatifu na ujuaji ni bora ungeuliza kwa nini huyo baba Diamond aliamua kuondoka na kumwacha mwanae. Kuna wanawake anaweza kukuambia jambo ukaondoka na suruali moja mazima, anyway tunatokea katika dini mbalimbali huenda uko sahihi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sentensi ni moja tu, dingi ni dingi tu!

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakuna kitu kama hicho ... niupuuzi mkubwa huu ..mzazi unapaswa kumlea mwanao nakumpatia mahitaji yake ya msingi yatakayo muweza kumpatia msukumo wakuweza kuzifikia ndoto zake ",

Hata kama ni mzazi masikini komaa na family yako ipatie matunzo hata kama ni haba na uionyeshe upendo" watoto wakija kukua wataelewa tu kwamba mzazi wetu ni masikini lakini hakuwahi kutu telekeza alikuwa pamoja nasi katika kila hali "

Sasa kama wewe ni mzazi halafu uliikimbia family yako" na kumuacha mtoto wako akipitia tabu za maisha ", hakika haustahiki kuonewa huruma na dunia .... acha yakukute mazito

Sent using Jamii Forums mobile app
 
So kama aliambiwa nakuondoka na hiyo suruali ndio amsuse mtoto wake ...hahaa dahh so sad"....... kwahiyo kinachotaka kumrejesha kwa mtoto sasa hivi ni nini " !?, zile hasira sasa hivi zimeisha !?, now ndio anatambua kuwa diamond ni mwanae !?

Umeshawahi jiuliza swali !?, kama diamond asingekuwa hivi alivyo leo baba yake angeendelea kumlilia lilia !?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…