ushauri wa bure kwa Jide juu ya redio ya watu

understanding

Member
Joined
Feb 17, 2013
Posts
75
Reaction score
34
Lad Jay Dee, The Pumpkin of the Old Homestead MUST NOT BE UPROOTED! maana halisi ya hiyo proverb ni USINYEE KAMBI. waswahili wanasema usisahau ulikotoka na aliyekutoa..

wanadamu tuna tabia ya kujisahau sana, haswa tupatapo mafanikio katika nyanja fulani zinazotuhusu. Kujisahau ni ugonjwa mkubwa tupatao sisi wanadamu. Lakini lazima tukubali kujisahau sio kuzuri, ebu jaribu kuvuta picha, hata tu ya kufikirika, vipi asingejitokeza yule mtu katika njia ya maisha yako, je leo ungekuwa hapo? ungekuwa ulivyo?

kamwe usijisahau kiasi cha kumtusi aliyekusimamisha, aliyekutoa katika aibu, aliyekufanya leo utembee na uonekane ulivyo...

Jide, redio ya watu ndio iliyokutoa, ndio waliokutambulisha katika anga ya muziki. maisha yako wewe ni matokeo ya moja kwa moja ya redio ya watu, leo ukitusi na kukebehi kiasi hicho ni kwamba hutafuti kingine zaidi ya laana.. wewe umeonekana kwa sababu ya redio ya watu, wale ndio waliokusimamisha, usisahau ulikotoka. Mumeo, kafundishwa ujanja na redio ya watu, kipaji chake kilionyeshwa na redio ya watu, ni redio ya watu ndio ilimlea na kumkuza. Biashara yenu, yaani Nyumbani Lounge, ni redio ya watu iliyotambulisha biashara yako, kumbuka, kumbuka fresh..... Leo mbona mnajisahau sana..

ushauri wangu: The Pumpkin of the Old Homestead MUST NOT BE UPROOTED!
 
Hide usisahau mchezo mliocheza na ruge south Africa hd ukatolewa kwny tuzo
 
Ukweli ni huuu jide bila clouds na clouds bila jide......

Unamkumbuka saida kaloli,mr.nice,kali p,daz nundaz,solo thang,east coast,gangwe mob,mr blue,top in dar,mangwea.

Uliza nani kafanya vizazi hivi vya music vipoteee......

Ni mume wa sister jide alishilikiana na ruge mtahaba na smooth vibe.

Leo zamu ya jide mnachonga poa jide namuheshimu sana na yeye analijua hilo luge namchukia sana na yeye na mawingu wanalijua hilo.

Ila ukweli ni kwamba biashara ya redio ndio hiyo na ruge ametusogeza sana na kufikia kujitambua sawa na ni sawa na kumchukia baba yako kwa matendo uliopitia utotoni.

Mtoto wa kilema hawezi kumuiga babaye kutembea!

Jide jipange na tafuta njia za kuzibiti mapato yako pasipo kubishana na mtu unauwezo wa kua na advocate kulipia kodi kujifanyia promo hata kwa mabango balabalani na sms mitandao na kuuza nyimbo online vyote vinawezekana bila ubishi.

Ruge hawezi na hakuwezi namwambia tena ruge kama alimshindwa sugu basi hamuwezi jide hasilani kwanini sisi tunamjua yeye mwizi na mnyang'anyi wa sanaa ya bongo tena kimbele mbele wa taifa kwa sasa!me namjua boss wake vema kwani alikua mtoto wa rafiki wa babu yangu wakati ule tupo iringa wao wali amia sisi ni kwetu....tuliwapokea na tukawakalimu jose ni mjanja sana ila anajua kuzuga sasa kama ni zamu yako jide usilie mbona mda sio mrefu nae dalali wa sanaa bongo anatemwa mawingu tena kinoma noma tunalijua sisi watu wa kazi tena kwa kashfa nzito....na atakimbilia ulaya au america we ngoja tuuu.

Usisahau jide kuwa nashukrani alafu usiwe na mbinu hizi tuu badilika njoo na mbinu mpya za mbali sio pale......

Pole gadna pole jide pole ruge kwa kumpoteza jide myajenge haraka.......

Jide usijidanganye na kimedia kama times kinaweza kukupa promo muulize kipenzi cha wamakonde 20% natunzo kibao!
 
sawasawa dada white the point is vinega wakiungana na Jide wafu fm lazima watoke povu.
 
Aaa ifike mahali km ulinisaidia basi kuna kitu na wewe ulifaidika bwana. Ni hizo nyimbo A jide pia zilifanya clouds ikapendwa. Sio kusimangana. Kwa hiyo mlimtoa nyie ndio mlikuwanasweat on stage?. Watu pia hawapendi kukosolewa, yawezekana hata clouds nao wamemnyonya sana, alipojistukia na kuachana nao wakaacha kupiga miziki yake. Komaa jd redio ziko nyingi sana, pia tv ya clouds na redio yao haina coverage nchi nzima
 
radio.ya wafu haina jipyA. jide big up kwa kuwachana.
 
Asilimia kubwa ya nyimbo za Jide zinahusu - Kasemwa/Kasengenywa/Watu hawamtakii mema/wachawi/mbona hazai na mengine mengi tu kwenye nyiimbo za huyu mwanadada kulikoni?
 
watanzania wanaogopa sana kuwa wakweli
kama ni ukweli ana haja gani kulaumiwa?
ukweli utakuweka huru
tuache unafiki bwana
 
Kama mnaweza tumpe masaa 24 ruge aondoke nnchini tena kwa kauli ya presidaaa jk......coz mda sio mrefu atapewa skendo ya kiufisadi ikulu subili tuu si anakimbelembel....nyie ngojeni ana mbwe,bwe kweli jamaaa.
 
Ni kweli uyasemayo mdau kwani kwa sasa kupitia clouds ndipo wengi wa wasanii walipotokea na baada ya kupata mafanikio kidogo ndipo wanapojisahau na bila kujua kwamba kufanikiwa sio mwisho wa matatizo yote Jide usiilaumu clouds kwa kutopiga kwao nyimbo yako uliyoitoa kwani huenda ni tatizo la kibinaadam tu
 

jana nimeuskia on satadei pawabrekifasti
 
Siku zote huwezi kuwa mtu bila watu.ila husikubali kunyanyasika kwa sbb ya fadhila ulizopewa.husiishi kwa kutegemea kumlinda yule aliyekufadhili.na kwatabia hiyo wewe najua ni ccm sbb hao ndio wanatabia ya kuwalinda wale walio washika mkono na kuwa onyesha njia na hata wakipotoka wataendelea kuwapongeza.kaka husiogope umaskini na husiwe mtumwa sbb ya fadhira.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…