Ushauri wa bure kwa "masupastaa"

Ushauri wa bure kwa "masupastaa"

TheChoji

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2009
Posts
5,771
Reaction score
17,849
Kuna mwanamuziki amewahi kusema "usupastaa ni zigo la misumari".

Unapokuwa supastaa, jamii inakuwa na haki ya kukusulubisha ipendavyo kwani wewe ni "public figure" na chochote unachofanya kinakua na public interest na watu wanaweza kukuchambua wapendavyo iwe kwa uzuri au kwa ubaya. Hiyo ndio "price" unayolipa kila siku kwa kuwa supastaa. Unapokua supastaa, tambua wewe ni mali ya umma!

Lakini sasa kumekuwa na tabia ya masupastaa wengi kudhani kwamba unapokua supastaa, basi na familia yako yote nao wanatakiwa "kushea" huo usupastaa wako. Tumeona masupastaa hasa wasanii wakiwaweka mama zao, baba zao, waume/wake zao, watoto wao nk katika "spotlight" hasa kwa kutumia mitandao ya kijamii bila kujua madhara yake.

Wanachosahau ni kwamba, unapomuweka mtu kwenye spotlight, huyo mtu naye anageuka mali ya umma na umma utaanza kumchambua bila kujali huyo mtu ni nani, ni wa jinsia gani au ana umri gani! Masupastaa wote waliowaweka watu wao wa karibu kwenye social media, mwisho wake hua ni watu hao kuaibishwa, kutukanwa, kuchambwa, kuwa "bullied", na kila aina ya matatizo. Wengi wa masupastaa hao huishia kuilaumu jamii wakidhani kwamba ndiyo yenye makosa, kumbe jamii inatekeleza haki yake ya msingi ya kuwasulubisha public figures! Yaani ni sawa na kumtupa mbuzi mbele ya kundi la mbwa-mwitu, halafu uje uwalaumu mbwa mwitu kwa kumrarua.

Wewe supastaa tambua kwamba wewe ni mali yetu, na zigo hili la misumari ni lazima ulibebe kwa kipindi chote utakachokua supastaa. Na yeyote utakaemleta mbele yetu awe ni mama yako, baba yako, mtoto wako, sisi kama jamii tutamsulubisha!

Njia pekee ya kuwaepusha watu uwapendao na suluba hiyo ni kuhakikisha unawaweka mbali na sisi kadri iwezekanavyo. Wapo masupastaa ambao wamefanikiwa kuweka familia zao mbali na kamwe huwezi kusikia jamii ikihangaika na watu hao. Do yourself and your family a favor, beba zigo lako la misumari peke yako, acha kuwabebesha zigo hilo watu wasiohusika.
 
Kuwa superstaa kuna vigezo vyake, na kwa hapa Tz supertaa hawazidi watano:

Moja ya vigezo, superstaa maisha yake na mipango yake sio ya kitaifa.
Hii ya maisha binafsi kuwa ya kitaifa ni ishara ya uchanga wa mtu kiakili. Kuna watu wana elimu kubwa, wazuri wa sura na maumbile, wana vitegauchumi vya maana, wana ndoa nzuri na a mfano na bado wako kimyaaa.

Sasa wewe una post picha ya mtoto wa kiume, ana rembua macho, sauti imelegea. Halafu unataka usifiwe eti handisamu!

#Ushoga hauji kama chafya
# wanawake wako wengi, msiwaongezee ushindani!
 
Kwa nchi za wenzetu, mtoto anaweza kumburuza mzazi wake mahakamani kwa kumpost kwenye mitandao na kusababisha awe embarrassed na public. Hii ni kwasababu mtoto hana uwezo wa kufanya maamuzi ya kuwa posted au la maana yeye bado ni tegemezi kwa mzazi. Hapo wa kulaumiwa au kushtakiwa ni huyo aliempost na sio jamii. Ubaya huku kwetu hata taasisi za kutetea haki za watoto sijui wanafanya kazi gani..?
 
Kuna mwanamuziki amewahi kusema "usupastaa ni zigo la misumari".

Unapokuwa supastaa, jamii inakuwa na haki ya kukusulubisha ipendavyo kwani wewe ni "public figure" na chochote unachofanya kinakua na public interest na watu wanaweza kukuchambua wapendavyo iwe kwa uzuri au kwa ubaya. Hiyo ndio "price" unayolipa kila siku kwa kuwa supastaa. Unapokua supastaa, tambua wewe ni mali ya umma!

Lakini sasa kumekuwa na tabia ya masupastaa wengi kudhani kwamba unapokua supastaa, basi na familia yako yote nao wanatakiwa "kushea" huo usupastaa wako. Tumeona masupastaa hasa wasanii wakiwaweka mama zao, baba zao, waume/wake zao, watoto wao nk katika "spotlight" hasa kwa kutumia mitandao ya kijamii bila kujua madhara yake.

Wanachosahau ni kwamba, unapomuweka mtu kwenye spotlight, huyo mtu naye anageuka mali ya umma na umma utaanza kumchambua bila kujali huyo mtu ni nani, ni wa jinsia gani au ana umri gani! Masupastaa wote waliowaweka watu wao wa karibu kwenye social media, mwisho wake hua ni watu hao kuaibishwa, kutukanwa, kuchambwa, kuwa "bullied", na kila aina ya matatizo. Wengi wa masupastaa hao huishia kuilaumu jamii wakidhani kwamba ndiyo yenye makosa, kumbe jamii inatekeleza haki yake ya msingi ya kuwasulubisha public figures! Yaani ni sawa na kumtupa mbuzi mbele ya kundi la mbwa-mwitu, halafu uje uwalaumu mbwa mwitu kwa kumrarua.

Wewe supastaa tambua kwamba wewe ni mali yetu, na zigo hili la misumari ni lazima ulibebe kwa kipindi chote utakachokua supastaa. Na yeyote utakaemleta mbele yetu awe ni mama yako, baba yako, mtoto wako, sisi kama jamii tutamsulubisha!

Njia pekee ya kuwaepusha watu uwapendao na suluba hiyo ni kuhakikisha unawaweka mbali na sisi kadri iwezekanavyo. Wapo masupastaa ambao wamefanikiwa kuweka familia zao mbali na kamwe huwezi kusikia jamii ikihangaika na watu hao. Do yourself and your family a favor, beba zigo lako la misumari peke yako, acha kuwabebesha zigo hilo watu wasiohusika.
Mkuu umenipa unondo maridhawa sana ,,jf is my mentor
 
Back
Top Bottom