Uko sawa mkuu,Hata mimi sijui kwa ninin hawa tbc wanafanya kitu namna hii. Watuhumiwa ni CDM, kwenye kutoa maelezo hawaitwi, wanaitwa watu wale wale, sasa sisi wanamchi ambao tbc ni ya kwetu, tutapata wapi maelezo ya upande wa wanaotuhumiwa?? Wabunge wa ccm walobaki bumngeni hawajadili huu muswada, na badala yake kila anayesimama ni kumshabulia MH. Tundu Lissu personally. Wengine wamekwenda mbali hata kuhoji weledi wake kwenye sheria, tena kwa kebehi. Mh Lissu ni msomi aliyebobea kwenye fani yake: WaTanzania wanajua hivyo na dunia nzima inajua hivyo!!Hii siyo haki kabisa,TBc angalieni mnachokifanya hakisaidii katika kumaliza utata huu. Kama alivyosema Machali wa NCCR, wananchi ndo wanaotaka muswada huu ungesomwa mara ya kwanza. Kwanini serikali ina haraka kupitisha?? Hii katiba ni ya wananchi na ndiyo wanaotaka washirikishwe katika hatua hii, kwa nini serikali inyoitwa "sikivu" imeziba masikio katika hili?? Kunakitu hapa. Tunawasubiri hao wabunge wa ccm warudi tuwaulize walikuwa wanawakilisha mawazo ya nani kwenye huu mchakato. Labda wote wabaki huko huko Dodoma au wakimbilie Dar kama walivyozoea.