USHAURI WA BURE:Swala Kuhusu Ufugaji wa Mifugo aina yoyote, Uliza hapa utapata Jibu bure

analysti

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2009
Posts
731
Reaction score
614
Hellow wana JF,

Nimetambua ukweli kuwa JF ni jukwaa linalowafikia watanzania waliowengi kirahisi hasa baada ya maendeleo makubwa ktk Sayansi na Teknolojia ktk nchi yetu.

Pia nimetambua kuwa JF inamchanganyiko wa watu wenye Taaluma mbalimbali ambazo tukizitumia vyema, basi JF inaweza kuwa ni jukwaa litakalokuwa na mchango mkubwa ktk kuyafikia malengo ya maendeleo ya Milenia (MDGs)

Mimi nikiwa kama Mtaalamu wa Mifugo. Nimeamua kuwasaidia watanzania wenzangu kwa kutumia utaalamu nilionao kupitia JF (kwa kushirikiana na wataalamu wa mifugo wengine waliomo humu JF). Natoa wito, kwa mtu yeyote aliye na swali kuhusiana na aspect yoyote ile ya Ufugaji, aulize hapa, ushauri utatolewa bure.Ushauri huu nitautoa mimi mwenyewe au Mtaalamu mwengine yeyote aliyemu humu kupitia uzi huu. Wafugaji wazoefu pia tunawa encourage kushare uzoefu wao ktk matatizo yatakayokuwa raised na wafugaji wengine.

Ninaamini Uzi huu utakuwa na manufaa kwa wafugaji na watu wengine ambao wangependa kufuga ili kujiongezea kipato, ukizingatia hali ya maisha inaendelea kuwa ngumu kadiri siku zinavyosonga mbele.

Karibuni!!
 
Nauliza, samaki aina ya tilapia (sato) wanafugwa kwa muda gani tangu wakiwa vifaranga (fingerlings) mpaka wawe wakubwa kwa kuuzwa (yaani wawe na uzito wa kilo1) bila ya kulishwa chakula chochote? (yaani wakue naturally)?
Thanks.
 
Jaribu kusoma hapa mkuu http://www.aquaticcommunity.com/tilapia/farming.php , kuna taarifa zote kuhusu Talapia farming, Kama utakwama sehemu usisite kuuliza.

Thanx
 
mkuu .... je upo tayari kwa maswali yahusuyo marketing/masoko yatokanayo na mifugo ?
 
Naomba kama unaziju dawa za kulisha ng,ombe wa nyama ili wakue kwa haraka nitajie na aina zake ikiwa ni pamoja na madhara yake au faida.
 
ni vyema sana umekuja na hili wazo lakini kwa kuwa wewe ni mtaalamu wa mifug mimi binafsi ningependa uweke kama mada fulani fulani hivi zinazohusu mifugo mbalimbali, mkwa mfano, unaweza ukaanza na mada ya ufugaji wa kuku wa kienyeji na wa kisasa, then ukafuata mada ya ng'ombe, nguruwe, samaki nk. kwa jinsi hiyo tutakuwa tunapata manufaa kwa kila aina ya mifugo utakayoweka hapa. from those issues, mtu anaweza kuchagua kitu gani afuge kutokana na jinsi ulivyelezana mazingira aliyopo.
natanguliza shukurani za dhati mkuu! Pamoja sana!
 
great .... kwanza kabisa .... hii program ya 'kilimo kwanza' naona tayari inabagua mifugo kama aina mojawapo ya farming ... nini maoni yako?

ninawaomba moderators wait-sticky hii thread .... it is of paramount merits to livestock farmers
 
Mimi nataka kufuga mbuzi je nitegemee changamoto zipi?
 
Asante mtaalamu kwa kujitolea, swali langu nina vifaranga 180 broiler wiki ya 3, wiki ya 1 waliumwa coccidiosis nikawatibia na Amprolium 5 days, je nitatakiwa kurudia tena matibabu, sipendi kuwa na dawa wiki za mwisho za kuuza, nitashukuru kwa ushauri
 
habari mkuu...mimi nina kuku wa kienyeji lakini juzi kuna mtetea mmoja ambaye alikuwa anataka alikuwa kama anapoteza nguvu za miguu na muda mwingi kuwa kama ananyongea lakini ukimshtua ana changamka kama wengine.jana nikasema ngoja nimkamate nimtengea na kumtibia kwa kumpa antibiotic lkn nilivyomkamata alikuwa vizuri tu lkn nilimuachia chini nikaona anajinyonganyonga na hatimaye akafa na mdomo akawa ametoa kama ute mzito hivi.nilikua naomba kujua hili tatizo linasababishwa na nini na matibabu yake ni yapi?Asante sana mkuu.
 
Hellow wana JF,

Nimetambua ukweli kuwa JF ni jukwaa linalowafikia watanzania waliowengi kirahisi hasa baada ya maendeleo makubwa ktk Sayansi na Teknolojia ktk nchi yetu.

Pia nimetambua kuwa JF inamchanganyiko wa watu wenye Taaluma mbalimbali ambazo tukizitumia vyema, basi JF inaweza kuwa ni jukwaa litakalokuwa na mchango mkubwa ktk kuyafikia malengo ya maendeleo ya Milenia (MDGs)

Mimi nikiwa kama Mtaalamu wa Mifugo. Nimeamua kuwasaidia watanzania wenzangu kwa kutumia utaalamu nilionao kupitia JF (kwa kushirikiana na wataalamu wa mifugo wengine waliomo humu JF). Natoa wito, kwa mtu yeyote aliye na swali kuhusiana na aspect yoyote ile ya Ufugaji, aulize hapa, ushauri utatolewa bure.Ushauri huu nitautoa mimi mwenyewe au Mtaalamu mwengine yeyote aliyemu humu kupitia uzi huu. Wafugaji wazoefu pia tunawa encourage kushare uzoefu wao ktk matatizo yatakayokuwa raised na wafugaji wengine.

Ninaamini Uzi huu utakuwa na manufaa kwa wafugaji na watu wengine ambao wangependa kufuga ili kujiongezea kipato, ukizingatia hali ya maisha inaendelea kuwa ngumu kadiri siku zinavyosonga mbele.

Karibuni!!
mimi ni mfugaji wa kuku wa kienyeji na nina vifaranga vingi sana ila kwa kama wiki sasa lazima vife 5au zaidi wanakuwa wanasinzia kama baridi vile mabawa yanateremka chini then anakufa jana tr 24 nikaenda vertenary wakanipa antibioti inaanza na oxy.......je hii ni dawa sahihi na je nikitaa hawa kuku wangu wasiugue ugue kila mara nafanyaje yaani niwape chanjo gani kwa muda gani nitafurahi sana kupata majibu napenda sana kufuga na sina utaalam nimeanza na kuku nataka nifuge mbuzi na ngombe pia. analysti
 
Last edited by a moderator:
Asante mtaalamu kwa kujitolea, swali langu nina vifaranga 180 broiler wiki ya 3, wiki ya 1 waliumwa coccidiosis nikawatibia na Amprolium 5 days, je nitatakiwa kurudia tena matibabu, sipendi kuwa na dawa wiki za mwisho za kuuza, nitashukuru kwa ushauri

Unakaribishwa sana mkuu,

Zingatia mambo yafuatayo:

1. Hakikisha banda lako haliwi na unyevunyevu kwenye maranda, utakapoona sehemu maji yamemwagika, basi toa maranda mahala hapo na weka mengine makavu. Hii inazuia kuota kwa vimelea vinavyosababisha coccidiosis.

2. Kwa sasa hivi, kila uamkapo asubuhi angalia bandani kama utaona kinyesi either chenye damu damu, au chenye rangi ya ugoro. Ukiona hivyo, hata kama ni sehemu moja, ni vyema kuku hao ukawaweka tena kwenye dose ya amprolium, kwa kuwa tayari watakuwa wameshapata maambukizi tena.

3. Kwa intake nyingine ya kuku, ni vyema ukazingatia ushauri No. 1 vizuri, na hakika coccidiosis halitokuwa tatizo kwako.

Nakutakia ufuganyi mwema wenye mafanikio!
 
habari mkuu...mimi nina kuku wa kienyeji lakini juzi kuna mtetea mmoja ambaye alikuwa anataka alikuwa kama anapoteza nguvu za miguu na muda mwingi kuwa kama ananyongea lakini ukimshtua ana changamka kama wengine.jana nikasema ngoja nimkamate nimtengea na kumtibia kwa kumpa antibiotic lkn nilivyomkamata alikuwa vizuri tu lkn nilimuachia chini nikaona anajinyonganyonga na hatimaye akafa na mdomo akawa ametoa kama ute mzito hivi.nilikua naomba kujua hili tatizo linasababishwa na nini na matibabu yake ni yapi?Asante sana mkuu.

Habari ni njema kiongozi!

Well kabla sijakwambia tatizo ni nini, naomba nifahamu mambo haya machache!

1. Una kuku wangapi hapo kwako?

2. Ni wangapi umewaona wana dalili kama hiyo, au hali ambayo unahisi si ya kawaida?

3. Kuku wako unawafungia ndani au wanazunguka nnje?, Kama unawafungia ndani unawalisha nini?

4. Kuna chanjo yoyote ile umewapa kuku wako? katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita?
 
Wapo kuku kama 50, nawafunga ndani lakini wanazunguka ndani ya fensi.yes nilipa chanjo ya new castle miez kama miwili na nusu iliyopita mkuu.
Nawalisha mchanganyiko wa pumba za mahindi, mahindi, mashudu, dagaa, mifupa na chokaa pia uwa nawapatia na majani atleast mara 3 kwa wiki.
Asante mkuu
 
mimi ni mfugaji wa kuku wa kienyeji na nina vifaranga vingi sana ila kwa kama wiki sasa lazima vife 5au zaidi wanakuwa wanasinzia kama baridi vile mabawa yanateremka chini then anakufa jana tr 24 nikaenda vertenary wakanipa antibioti inaanza na oxy.......je hii ni dawa sahihi na je nikitaa hawa kuku wangu wasiugue ugue kila mara nafanyaje yaani niwape chanjo gani kwa muda gani nitafurahi sana kupata majibu napenda sana kufuga na sina utaalam nimeanza na kuku nataka nifuge mbuzi na ngombe pia. analysti

Well!

Hiyo ni dawa sahihi tu,But

kama kuku wako hawa unawafungia ndani, nina maana kama siyo kuku wanaozunguka wenyewe, basi angalia kinyesi chao, kama kina streaks za damu au ni cha brown, kama kina appear hivyo, wape Amprolium kwa siku tano. Kama ni Cheupe na wanaharisha, endelea na OTC (Oxytetracycline). Na hata kama ni otherwise, endelea tu na OTC.

Chanjo:
Tatizo kubwa linalosumbua kuku wa kienyeji Tanzania ni Mdondo (Newcastle Disease (NCD)), Hivyo kuwachanja kuku dhidi ya NCD is Mandatory kama unahitaji mafanikio. Kwa kutegemeana na wingi wa vifaranga unaweza kununua chanjo ya mdondo ya maji au ya matone. Kama ni wengi tumia ya kuweka kwenye maji, kama ni wachache tumia ya matone. Faida ya chanjo ya matone ni kwamba yenyewe ni thermostable, kwa maana kwamba inauwezo wa kustahimili joto pasipokuharibika, ukisha nunua unachanja kuku wako, then unaitunza kwenye jokofu, na utaitumia unapochanja tena. Chanjo ya kuweka kwenye maji ni single use.

Chanja kuku wakiwa na siku saba, rudia wakifikisha siku 21, baada ya hapo chanja kila baada yamiezi mi tatu.

Usisite kwa maswali ya nyongeza!! Hakuna Muongozo wa spika!!
 
Back
Top Bottom