Ushauri wa Da Muna ni mzuri msiubeze

Ushauri wa Da Muna ni mzuri msiubeze

cutelove

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2017
Posts
3,448
Reaction score
7,972
Kwanza pole kwa Da Muna kwa matatizo yaliyompata

Da Muna akiongea na wanandishi wa habari alisema kitu kwa wanawake ambacho tunatakiwa kuwa na tahadhari nacho..alisema wanawake tuwe makini tunapoingia kwenye mahusiano na mwanaume huku una ujauzito au mtoto wa mwanaume mwingine

Kweli hapa wanawake huwa tunakosea sana,na nadhani Da Muna amewapa wasichana au wanawake wenye watoto wadogo au wenye ujauzito hata kama mmependana na mwanaume kiasi gani usije ukahamisha ujauzito au mtoto kuwa mtoto wa mwanaume mwingine ambaye sio baba halisi wa mtoto eti itakuwa siri ya nyinyi wawili

Siku mtoto akipata majanga ndo utajuta,kuna wanaume wengine atakwambia mpeleke kwa baba yake hii sio damu yangu,ndo utajuta kuzaliwa

Wanaume ni wazuri kama ana uhakika asilimia 100 kuwa mtoto ni wake ila ni wabaya akijua mtoto si wake hata kama mlifanya siri ya kubadilisha umiliki wa mtoto,siku yakikuta utajuta
 
Na kwanini uingie kwenye mahusiano mengine ukiwa na mimba ya MTU mwingine bila kutoa taarifa kwa MTU mpya?
Hapo chacha halafu badae unakuja kulialia na kuanza kutoa ushauri eti
 
Back
Top Bottom