Ushauri wa eneo la kufanyia Biashara ya Ufundi simu

Ushauri wa eneo la kufanyia Biashara ya Ufundi simu

Circuit Breaker

Senior Member
Joined
Mar 31, 2021
Posts
158
Reaction score
347
WanajamiiForums habari za saa hizi.

Nipo hapa naomba ushauri wa location ya kufungua Biashara ya Ufundi simu.

Mimi nikija niliemaliza chuo mwaka huu 2021, ukiachana na tahaluma niliyosomea chuo pia nina ujuzi wa ufundi simu, kwa upande wa hardware na software. Nina mpango wa kufungua ofisi ya ufundi simu ambapo natarajia kukodi fremu kwa garama ya 100,000-120,000 eneo lililochangamka kwa hapa jijini Dar es Salaam.

Kwa mawazo yangu niliwaza nifungue office Gongolamboto, maeneo ya stendi karibu na soko, kwa sababu ya muingiliano wa watu, ila nikaona niombe kwanza ushauri hapa JF naweza nikapata wazo mbadala la sehemu ya kufanyia hii biashara.

20211023_234518.jpg

Sent from my SM-G570F using JamiiForums mobile app
 
Kwa maeneo mbali na kkoo kuna changamoto moja kubwa ni upatikanaji wa spare za kifaa husika.

Yaani unawezaletewa simu mbovu kibati, ukafungua kwenda kwa kuchoma nauli kukipata kkoo ni jambo ambalo halihusiani kabisa na feedback kwa mteja, yeye ili akulipe mpaka kifaa chake kipone.

Bado kufunga kisifanye kwa ufanisi unaotakiwa[emoji38][emoji38], yaani ni bora ukajibanze hapo hapo kkoo.
 
Tatizo sitoweza kupata frem Kariakoo.

Pia ofisi nayofungua nataka ikue na hata tahaluma yangu nita practice hapo hapo kwenye office moja (nimesoma Umeme/Electrical).

Pia nitaongeza huduma za kifedha kama NMB, CRDB, tigo pesa, mpesa etc with time. ndo sababu ya mimi kutaka kwenda maali nitakapopaweza kwa maana ya kupata frem nitakayoweza kulipia kwa kuanzia.
 
Kachukuwe ofisi pale kwenye jengo la machinga complex ni kama vile upo kariakoo tu nadhani kwa bei hiyo unaeza pata vizuri tu,Nijuavo ofisi ya simu haihitaji ofisi kubwa sana.
 
Kachukuwe ofisi pale kwenye jengo la machinga complex ni kama vile upo kariakoo tu nadhani kwa bei hiyo unaeza pata vizuri tu,Nijuavo ofisi ya simu haihitaji ofisi kubwa sana.
Asante mkuu, nitaenda kufanya research kidogo hapo
 
Ni exactly mwaka mmoja sasa umepita tangu nilipoomba ushauri humu.
Nilifanya issues nyingine kabla ya kuanza hili swala la ufundi sim, nimefungua ofisi kibada kigamboni ni ofisi mpya ina mwezi mmoja sasa.
Asanteni sana kwa ushauri,
Kioo cha samsung a11 shingapi fundi
 
Back
Top Bottom