Jibaba Bonge
JF-Expert Member
- May 6, 2008
- 1,246
- 402
Hii imetokea Dar. Dada mmoja amekuwa akiuguliwa na mume wake ugonjwa ambao ilibidi afanyiwe operation (medium). Pamoja na kwamba operation ilikuwa successful mume aligundulika kuwa ana ngoma (HIV+), ilibidi na huyo mdada ashauriwa na madaktari kupima, akakutwa negative.
Amemuendea spouse wangu kumuomba ushauri, kwamba aendelee na hiyo ndoa au aivunge. kama akiendelea nayo maana yake mahusiano ya mke na mume yataendela na kama hatakubali hayo mahusiano then ndoa iko mashakani. Spouse wangu ameshindwa kumshauri na mimi pia nimeshindwa.
Wana JF tusaidieni mawazo namna ya kumshauri huyu dada,
Dah...! Hadi JIBABA ameshindwa kutoa ushauri....!Hii imetokea Dar. Dada mmoja amekuwa akiuguliwa na mume wake ugonjwa ambao ilibidi afanyiwe operation (medium). Pamoja na kwamba operation ilikuwa successful mume aligundulika kuwa ana ngoma (HIV+), ilibidi na huyo mdada ashauriwa na madaktari kupima, akakutwa negative.
Amemuendea spouse wangu kumuomba ushauri, kwamba aendelee na hiyo ndoa au aivunge. kama akiendelea nayo maana yake mahusiano ya mke na mume yataendela na kama hatakubali hayo mahusiano then ndoa iko mashakani. Spouse wangu ameshindwa kumshauri na mimi pia nimeshindwa.
Wana JF tusaidieni mawazo namna ya kumshauri huyu dada,
nimekurekebisha kiswahili chako hapo juuDah...! Hadi JIBABA ameshindwa kutoa ushauri....!
Aidha, mimi ningemshuri asivunje ndoa yake, bali akae chini na mmewe wajadili ripoti hiyo ya madaktari, na namna ya kuendelea na maisha. Hii ni iwapo tayari wameshazaa, na wana watoto sasa. La msingi ni kuwa makini sana na muangalifu sana katika mahusiano yao.
Achunguze kama jamaa alipata kujua kuwa ameadhirikakabla, na iwapo alijua, lakini hakuwa wazi, basi ni vema akavunja hiyo ndoa bila huruma, lakini kama aliwahi kuwa muwazi kwa upositive wake, au hakuwahi kujua kama ameadhirika, then the above advice may apply...!ameathirika uh!
Kama hawana watoto, then ni vizuri akaangalia maisha yake kwa utangulizi zaidi, japo mawazo ya jamaa nayo yapewe nafasi....!
Aidha, pole zimfikie na amkaribishe Mungu katika maisha yake yote...!