Ushauri wa kibiashara,mtaji wa tsh. Million 30

Huyo kaka yako ana matatizo, anawezaje kukupa au kukukopesha hela ya mtaji wa biashara isiyojulika. Labda hizo hela ni chafu.

Huyu kaka hana matatizo ya akili kama usemavyo,nakanusha hiyo kauli yako...naomba nieleweke kuwa mtaji wa mil 30 upo tayari ila kwa bahati mbaya sina idea tofaut tofaut zitakazoniwezesha kuizungusha hiyo pesa. ndo mana nkaja JF kuomba ushauri maana natambua kuwa watu humu ndani wana idea nyingi tena zilizo tofauti.,so naweza nikapata idea ambayo sikuwa naitambua kabla na ikawa ndo chachu ya maendeleo. ndg Buza nami ni hayo tu.
 
Unapenda kilimo (hapa nikimaanisha pamoja na ufugaji)? if yes, ni pm location yako na interests ulizonazo plus kazi uliyosomea at least ninaweza nikakushauri kitu... Hata hiyo mil 30 itakua nyingi.
 
Kabla cjatoa ushauri wangu naomba kukuuliza umesomea fani ipi??
 
Kabla cjatoa ushauri wangu naomba kukuuliza umesomea fani ipi??

Mimi nimesomea masuala ya Development Studies..karibu kwa ushauru, ushauri wako ni wa muhimu
 
Uko wapi?? Kama uko mjini tafuta sehemu yenye ofisi nyingi then fungua stationary..target kuwauzia watu wa maofisini kwa jumla na reja reja anza kujipendekeza kwa watu wa ofisini kama wewe ni mwanamke itakuwa rahisi kwako kupata connection

Kuna wanaume humu wana wish wangelikuwa wanawake. Duh!
 
Kuna wanaume humu wana wish wangelikuwa wanawake. Duh!

Hayo umesema wewe mimi nampa tu according na reality ya maisha ya downtown Dar Es Salaam
Ukianza kunishambulia mimi sina la kukurudishia but nitakudharau
 
Hayo umesema wewe mimi nampa tu according na reality ya maisha ya downtown Dar Es Salaam
Ukianza kunishambulia mimi sina la kukurudishia but nitakudharau

Nakuruhusu unidharau kama ukinipa sababu positive kwamba mtu kuwa mwanamke ni advantage kwenye biashara. Je nikwamba wafanya biashara wengi upendelea kutoa biashara kwa wanawake? kwa sababu kama ni hivyo namimi nitapenda kuwa mwanamke. Nadhani ukiri makosa uombe msamaha na u withdraw hiyo statement. Inaruhusiwa kufanya hivyo
 
Niombe msamaha kwa kipi?? Wakati ndio reality.. Take it or leave it...
Anayeanzisha business hiyo ndio atajua pumba ni zipi na mchele ni upi
 
Ndg. Bobo ninachoshangaa ni kuwa Huyo kaka yako amekupa Sh 30m bila hata kukuuliza unachotaka kufanya. Nikuulize biashara gani wewe unapenda kufanya?. Biashara ziko nyingi sana na kila biashara kuna watu zimewatajirisha. Hoja siyo kufanya tu biashara Fulani kwasababu ina faida kubwa, chamsingi ni kufanya biashara unayoipenda. Kama biashara huipendi lakini unaifanya tu kwasababu umeambiwa Ina faida sana ujue utakata msingi tu.
 
Tafuta thread zenye michango na mtazamo kama wa kwako ziko nyingi tuu umu JF kama Micha
alivyochangia...
Na nakushauri sio kila ushauri ni wa kuufata au kukumiza kichwa kwa majibuya wachangiaji wengine ni wivu tuu ndio unawasumbua,,,kwa kuwa wana muhuri ya wivu wasiotaka wenzao waendelee lazima watajitahidi kuwarudisha nyuma
 
Nashukuru sana ndg Chum chang...hilo nalo sijaliaacha nimeeanza kufuatilia thread kadhaa ambazo nazo zina mtazamo yakinifu kama wangu..na zaidi ya yote bado nachanganua na nitatoa feedback kwa kile nilichoamua. nashukuru sana
 
Naomba unielewe ndg Buza. mtaji wa mil 30 upo tayari..swali ni jinsi ya kupata wazo la biashara ambalo litaweza kusaidia kuweza kuizungusha hiyo pesa na kuweza kurudisha mtaji niliopatiwa. hoja ni kufanya biashara yenye faida isiyokuwa na walakini ndani yake, i mean isiyo na magendo yenye uhalali kabisa. ndo mana nipo hapa kwa ushauri pamoja na wazo ambalo unaona litakuwa ni tija kwa maendeleo kutokana na mtaji husika hapo juu. nashukuru kwa ushauri
 
Nashukuru sana ndg Chum chang...hilo nalo sijaliaacha nimeeanza kufuatilia thread kadhaa ambazo nazo zina mtazamo yakinifu kama wangu..na zaidi ya yote bado nachanganua na nitatoa feedback kwa kile nilichoamua. nashukuru sana
Yap ukirudi na kutoa feedback huo ndio ungwana-mimi si nabii lkn nakutabiria mafanikio na nakuombea kila kheri kwenye safari hiyo unayotaka kuianzisha iwe na mafanikio na uwezi kukabiliana na yatakayo jitokeza,wenzio tulipita umo umo
 
we kweli bobo
 
Good argument.
 
Yap ukirudi na kutoa feedback huo ndio ungwana-mimi si nabii lkn nakutabiria mafanikio na nakuombea kila kheri kwenye safari hiyo unayotaka kuianzisha iwe na mafanikio na uwezi kukabiliana na yatakayo jitokeza,wenzio tulipita umo umo

shukurani mkuu...nitarudi tena kutoa feedback ya kile nlichokipata ili iwe chachu kwa vijana wenzangu wenye mtazamo kama wangu...inshallah.!!
 
Uko wapi?? Kama uko mjini tafuta sehemu yenye ofisi nyingi then fungua stationary..target kuwauzia watu wa maofisini kwa jumla na reja reja anza kujipendekeza kwa watu wa ofisini kama wewe ni mwanamke itakuwa rahisi kwako kupata connection
Red: unamaanisha ana 'uchumi'?
 
Huyo kaka yako ni mfanyakazi au mjasiriamali?kama ni mjasiriamali anafanya shughuli gani?manake unaweza kuungana na huyo kaka yako kama ni mjasiriamali mkafanya hiyo biashara yake pamoja iliyoweza kumpa faida ya kukukopesha wewe.
 
Fungua internet cafe na pemben yake stationary,unaeza ukaanza na comp 10 desk top,printer scanner,photocopy machine,n.k
cafe goes together with stationary kwa mjin inalipa
you can take this or leave it
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…