Ushauri wa kisheria; je tukiamua tukate rufaa na yeye akienda mahakaman hatima yake ni nini?

sam2015

Senior Member
Joined
Dec 20, 2015
Posts
107
Reaction score
112
Wadau mliosoma sheria naomba ushauri kuna ndugu yangu anakesi ya miradhi aliyoifungua, ambayo imechukua muda wa miaka mitatu hukumu imetoka juzi na ndugu yangu ameshidwa.

Kutokana na kesi ilivyoendeshwa tunaona mahakama haijamtendea haki kwani mlalamikiwa ni mke wa marehemu ambaye hajazaa mtoto mtoto na marehemu.

Mlalamikaji (mtoto) ambaye ni ndugu yangu ni mtoto halali wa kuzaliwa wa marehemu pamoja na ushahidi uliotolewa na ndugu wa marehemu wakimewo wajomba,baba wadogo na mashangazi lkn ameshidwa kesi.

Hakimu amekataa cheti cha ndoa cha mzazi wa mtoto na kumpa haki malalamikiwa.

Sasa mtoto ameamua kukata rufaa lkn mlalamikiwa amemtishia endapo atakata rufaa na yeye atafungua kesi ya KUGUSHI ya hati ya ndoa aliyotumia mama yake kwa kuwa wakati ndoa inafugwa taarifa zake hazijasajiliwa RITA.

Sasa hofu yetu mama ni mtumishi wa umma , je tukiamua tukate rufaa na yeye akienda mahakaman hatima yake ni nini USHAURI
 
Kuwa mtoto wa marehemu haitegemei cheti, cha ndoa cha mama yake..!
 
Kata rufaaa haraka hiyo ya jinai haina mashiko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…