stwita
JF-Expert Member
- Feb 14, 2011
- 1,340
- 760
Endapo wachumba (watu wazima zaidi ya miaka 18) wamefunga ndoa ya kiserikali kwa siri (bila ndugu wa pande zote kutaarifiwa), ikiwa ni shinikizo/sharti la mchumba wa kiume, kwamba ili atoe mahari kwa wazazi wa mwanamke na kabla ya kufunga ndoa msikitini/kanisani, lazima mwanamke akubali kwanza kufunga ndoa ya kiserikali (na iwe siri kati yao na mashahidi wao tu). Mwanamke anakubali kufuata masharti hayo (ingawa hakubaliani na wazo hilo) na ndoa inafungwa bomani. Kutokana na ugumu wa masharti hayo mmoja wa wanandoa anapata na athari za kisaikolojia (msongo wa mawazo) na hawafanyi tendo la ndoa toka siku ya ndoa na kuendelea siku za mbele hadi miezi kadhaa inapita (na hivyo ndoa kutotimizwa). Kutokana na sababu zote zilizotajwa , wanandoa hawaishi pamoja na wala hawawezi kuishi pamoja kwani hawana maelewano tena na wamekuwa maadui (na, hata hivyo, mpango wa kuishi pamoja haukuwepo tangu mwanzo kwani ndoa ilikuwa ya siri). Je ndoa hii ni batili au batilifu? Inaweza kutenguliwa na mahakama kama mmojawao atalalamika?Taratibu zipi zifuatwe ili shauri lipelekwe mahakamani? Inaweza kuchukua muda gani hadi ndoa kutenguliwa (kama ni ya kutenguliwa)?