Ushauri wa kiufundi katika utanuaji na ukarabati wa maghorofa pasipo kuleta madhara

Samico Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Feb 6, 2022
Posts
486
Reaction score
1,237
Habari wadau, wamiliki, watumiaji na wasimamizi wote katika sekta ya ujenzi.

Kwanza nitoe pole kwa wahanga waliokutwa na jambo zito la kuangukiwa na ghorofa kariakoo!

Naomba kutoa machache kutokana na uzoefu wangu kiufundi katika majengo makubwa na madogo!

Kwanza kabisa Siyo kosa kiufundi jengo lolote lililojengwa zamani kuboreshwa.

Yapo maboresho ya aina nyingi katika jengo! Mfano

1. Maboresho ya inje (rangi, vioo, n.k)
2. Maboresho ya mifumo (Mifumo ya maji, umeme, lift n.k)
3. Maboresho ya umbo la jengo (Hii inahusisha kubadili umbile la jengo either kwa kuongeza vyumba, kuongeza msingi, au maboresho yoyote yanayogusa mhimili wa jengo n.k)

Maboresho yote yote hapo juu yanaweza kufanyika kwa kuzingatia taratibu za ujenzi.

LAKINI ZINGATIO KUU, Siyo kila fundi ujenzi/Mkandarasi anaweza kufanya ukarabati unaogusa mihimili mikuu ya jengo (nguzo au kuta kuu)

Nimefanya kazi za ufundi na watu kutoka mataifa mbalimbali kuna machache nimejifunza ambayo nashauri mamlaka zetu ziyafanyie kazi!
Ujenzi ni kama kuotesha mti, na maboresho makuu ni kama kuhamisha mti huo ukiwa hai na uhakikisha haufi na unakuwa bora.

Maeneo ya mijini hasa sehemu mhimu kama kariakoo ambako majengo binafsi yanatumiwa na umma kwa sehemu kubwa!

Maboresho yake katika mihimili mikuu ya jengo nashsuri yafanywe namna hii.

1.Watumie Fundi maalum aliyeidhinishwa/ Kampuni maalum (ya ndani au inje ya nchi) ambao watakuwa shortlisted na mamlaka baada ya kuchunjwa!

Hivyo mmiliki wa jengo anapohitaji kufanya maboresho ya umbo la jengo mamlaka mpeni orodha ya fundi anaetakiwa kumtumia ambae atazingatia taratibu za ujenzi pasipo madhara.

2. AU Maboresho yanayogusa jengo katika majengo ya biashara yafanywe na mamlaka za ujenzi ( mfano TBA n.k); Mteja apewe tathmini ya gharama alipie.

3. Jengo lolote linalotaka kufanyiwa maboresho makubwa lifungwe liwe tupu (pasifanyike biashara yoyote katika eneo hilo kwa muda wote wa ukarabati.
4.Taratibu zote za ukaguzi zingatiwe na mamlaka katika hatua zote kama ilivyo katika ujenzi wa jengo jipya!
5. Anaeshindwa kukubali masharti hayo ya ukarabati ni bora aache kabisa.

Kuliko kujenga kinyemela, Watu wote wanaobainika kutoa nyaraka za vibali kinyume na taratibu hatua kali zichukuliwe ikiwemo kunyongwa, kufukuzwa kazi au kufutiwa leseni au jengo kutaifishwa liwe chini ya NHC

IFAHAMIKE WAZI kwamba;

  • Kazi ya maboresho ya mhimili wa jengo huwa inahitaji akili nyingi, vifaa maalum kuliko hata kujenga jengo jipya kiusalama!
  • Kazi ya kuongeza urefu wa kina cha jengo au msingi wa ghorofa hauna shortcut ni lazima uweke nguzo imara ili kutoa nguzo dhaifu, ni lazima uweke msingi imara ili kutoa msingi dhaifu! Mambo kama haya Siyo kila fundi anaweza!
Wamiliki na wasimamizi wa majengo watambue hili ; Tamaa mbele mauti nyuma, Mtaka vyote hukosa vyote!

Tunaweza kuregeza sheria majengo ya makazi binafsi huko mtaani lakini kwa majengo mhimu na ya kibiashara kama ya kariakoo sheria isiwe na simile!

Haya ni maoni yangu fundi Samico, mbobevu wa masuala ya ujenzi na umeme!
 
Rushwaaaaaa.....x 1000
 
Vipi usalama wa majengo yaliyokwisha chimbuliwa tayali yanatumika! Nini maoni yako bwana fundi maana naogopa hata kwenda kariakoo sasa
 
Tusiwe na wasiwasi Ukarabati unafanywa duniani kote! Kama ujenzi umefuata na kuzingatia vigezo jengo ni vigumu sana kuanguka!

Hizi hapa ndiyo sababu kuu zinazoweza kuangusha jengo

1. Makosa ya kiufundi wakati wa ujenzi
2. Majanga mithili ya kimbuka au tetemeko n.k yanaweza kuchangia kuangusha jengo lililokosewa katika usanifu!

Inje sababu kuu hakuna jengo linaweza kuanguka ambalo limekwisha kujengwa!
 
Kwahiyo fundi unatuamisha kwamba wakijenga hao uliowataja hakuna jengo litaanguka?
Jengo lililozingatia ubora haliwezi kuanguka!
Pia jengo dhaifu linaweza kuanguka wakati wa ujenzi lakini baada ya ujenzi linavyozidi kukauka huongeza ubora katika udhaifu wake wa awali! Hivyo haliwezi kuanguka kama hakutakuwa na majanga au matumizi kupita uwezo wake
 
Back
Top Bottom