CHADEMA kinatoa changamoto tu kwa CCM lakini si chama adui au ndo hatutakaa meza moja, kwa sasa tunakoenda tutatafuta kukaa meza moja kila mara, hatuhitaji muafaka hapa miaka mitano hii tunahitaji kujadili hoja, kukosoana kisera na kiutendaji, na kushawishi wananchi nani anafaa kuingia Ikulu 2015 kuweka mambo sawa bila aibu. Ukicheki matokeo itakuwa ni aibu sana kama chama chochote kitaibuka na kuanza kukisengenya kingine, wote hakuna aliepata kura za ajabu. Kuna mgawanyiko mkubwa wa maoni. CHADEMA kaza buti, CCM jirekebishe, CUF na wengine ongezeni juhudi. Wote acheni visa sasa na kushutumiana, pale mlipokosea mkiri ni uungwana na mtueleze mikakati yenu kuweka mambo sawa.