Umeshavuna? Tupe uzoefu
Vitunguu machungu yake ni mtaji si chini ya milioni 2 kwa ekari moja na ukitoa zigo kubwa la ekari zaidi ya 100 ukataka usubiri bei iwe nzuri hifadhi yake ni kasheshe, lazima ujenge chanja zake na kwa eneo lako eka 200 ni parefu hapo, hivyo jitazame urefu wa mtaji wako otherwise kitunguu kinalipa na Kilosa ni kwake.
Looks like wakulima watarajiwa tunaweza kujifunza mengi sana kutoka kwako Mr. Kubota. Tutaomba uwe unafunguka kadri uwezavyo unapost mkuu. Thanks indvance!
Na mimi nafikiria kununua ardhi nzuri kama ekari 50 hivi za kuanzia. Naufuatilia huu uzi kwa makini sana. Niko interested kupanda mazao ya kudumu kama machungwa ao maembe.
Changamoto inyoninyima usingizi ni ulinzi wa mazao hasa pale yanapokuwa tayari. Udhibiti wake uko vipi especially ukiwa na shamba la ekari 100?
Karibu mgama, jimboni kwa Mh. Mgimwa tulime njegere
Mkuu Bobby asante kwa comments zako. Dunia imejaza mengi mazuri yakimsubiri yeyote yule ayatafutae! FINDING is reserved to those who SEARCH !! Abishaye hodi ndiye hufunguliwa! Anaekuwa mdadisi sana kuuliza anachotaka kujua ndiye anaezoa majibu mengi sana. Dunia itafunguka kwake atafutaye, badala ya kusubiri kama mvua, sometimes mvua miaka mingine huwa hainyeshi sana. Mkuu kama kunaishu unataka kujua undani wake uliza tu, wengi watafunguka sana kwa kina kirefu tu!
Mkuu Bobby unatisha!! Yes late Jim Rhon, nadhani hujasahau kilichomfanya akasilike na kuanza kupambana na umasikini, aliposhindwa kununua candy ikiuzwa dola 2. Mkuu Bobby tuko pamoja sana.Kubota umemaliza kila kitu kwenye hii post. I see something common between us kwenye maneno yako, bila shaka wewe ni mfuatiliaji mzuri wa watu kama the late Jim Rhon, he is actually one of my favorites. Avatar yako iko so inspiring, kwangu mimi kilimo ni hobbie in the first place lakini nataka kinizalishie pia. Hakuna kitu kizuri kama kutengeneza pesa kwa kufanya kile unachokipenda someone said the other day kwamba siri ya kuishi maisha yenye mafanikio is to "to find what you love doing then make it pay for you". Nitakusumbua sana wewe na wengineo kwenye hii issue ya kilimo na Im glad uko tayari kwa hilo.
Mkuu VUVUZELA suala la ulinzi ni muhimu sana na linahitaji uerevu sana. Kutokana na umuhimu wa suala hili Mkuu kama utaona inafaa nakushauri uifanye hii post yako iwe thread kamili ijitegemee ili ipate uzito wengi wachangie tupate mwelekeo maana kwa ilivyo hapa imemezwa wengi hawataiona na inaweza isijadiliwe. Sijawahi kukutana na mjadala unaohusu ulinzi humu, siku zote tunaongelea kukusanya na kuzalisha mali tu. Na mimi nimetega hapa kusikiliza mauzoefu si unajua JF kisima cha maarifa.Na mimi nafikiria kununua ardhi nzuri kama ekari 50 hivi za kuanzia. Naufuatilia huu uzi kwa makini sana. Niko interested kupanda mazao ya kudumu kama machungwa ao maembe.
Changamoto inyoninyima usingizi ni ulinzi wa mazao hasa pale yanapokuwa tayari. Udhibiti wake uko vipi especially ukiwa na shamba la ekari 100?