Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Habari zenu! Naomba msaada wa taarifa zitakazosaidia kufungua daycare. Mtu anahitaji kua na nini na nini kwa standard day care, natanguliza shukrani
Dah! Nimechekaje? Eti nitafunga kwenye kambaPia nakushauri uwe angalau na Diploma ya mambo ya Lishe.
La sivyo utauwa watoto wa watu,nakuwatoa vitambi
Na pili ulezi ni kipaji,kuna mama alifungua hii kila siku alikuwa anapigizana kelele na watoto,anawafokea kama kichaa.
Yaani tambua kwamba ile ni ajira,sio unavyomlea mwanao ufanye kama unavyolea watoto hao.
Kuna Dar Care moja pale Tabata,yaani kwa jinsi malezi yalivyo vizuri basi unakuta unaenda kumchukua mtoto anakugomea hataki kuondoka,hadi umdanganye ndio unaendanae nyumbani,kesho mapema tu analianzisha tena aende Care Center.
Sasa lazima ujue namna ya kukaa na watoto,kuna watoto wamepinda kwa utundu.na pia jitambue kama kweli unaweza na usibahatishe.
Maana mie binafsi sio siri siwezi kabisaa,yaani watakuta siku moja nimewafunga kamba watoto wote,yaani pale ukienda kuna watoto kama wamekula nyama ya Tumbili,ukimwambia aache hiki kashika kile,kupiga wenzao,rushia mawe wenzake,yaani balaa,bora wale wachanga,lakini wakiishafika 3 yrs ni balaa bin wazim.