Mkuu kwenye gpu rendering kila kampuni inakuwa na Accelerators zake, Ya intel inaitwa Quicksync, Nvidia ni NvenC na Amd ana VCE.
Mara nyingi Nvidia anakuwa vizuri zaidi ila hio Quicksync ya intel ina value zaidi sababu unaipata kwenye machine yoyote yenye intel HD, sema nzuri zaidi ni kuanzia gen ya 11 ama gpu zao za Arc.
Hivyo kama unatumia Accelerators combo ya intel+Nvidia kwa budget ndogo ni nzuri.
Gpu nyingi za Nvidia zina Nvenc mpaka za zamani kama Gtx 750ti, sema zinatofautiana version mfano 750ti inakubali codecs za kizamani kama X264 ila codecs mpya kama Hevc/X265 na Av1 haikubali.
Sasa unaangalia mwenyewe matumizi kama unagota x264 gtx 750ti kupanda, kama unagota x265 ni gtx 1050ti kupanda na kama unataka Av1 basi hizi Rtx 40xx mpya zinapiga codecs zote.
Ila kama upo serious zaidi huwa best way ni kutumia Cpu, tafuta Ryzen ama Intel Gen 12 kupanda zenye core nyingi kadri iwezekanavyo.