Sikiliza hii story ita kumotivate kidogo kama una nia.
Niliacha shule September 2013 nikiwa form one nikaendelea na Mishe mtaani mambo yalipokuwa magumu mtaani nikarudi shule 2019 kuanza QT but nilijitoa kwa hali na Mali kusoma na nikawa mwanafunzi kweli nikawa nasoma masomo yote kumi 2019 nikafanya paper la QT nika pass 2020 nikajisajili form four nikiwa Naendelea kusoma masomo yote 10, nikafanya paper la form four nikapata division one ya 12 nikifeli hesabu na fizikia kwa kupata "F" pekee huku kemia nikiwa na D na biology C lakini masomo yote ta arts ni A na B pekee sina C kwenye somo la art hata Moja.
2021 nikaanza form five na six kwa Mwaka mmoja nikijisajili kwa kombi ya HGL Mwaka huu mwezi wa tano nikafanya paper nikapata division one ya 8, mpaka muda huu Niko chuo Mwaka wa kwanza na boom juu.
Kwaiyo nimesoma madarasa 6 kwa miaka 3 na Niko chuo kikuu.
Hivyo basi kama uko willing anza kujiandaa kiuchumi na ujitoe hasa kusoma kufaulu inawezekana nimekuwekea matokeo yangu ya sayansi na matokeo yalikua sio poa sana kulingana na mzigo wa masomo mengi niliobeba na ugumu kwa hayo masomo ya sayansi hivyo nikushauri uchukue masomo nane History, English, kiswahil, mathematics, biology, civics, geography na literature.
Kila la kheri.
Sent from my TECNO K7 using
JamiiForums mobile app