Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,692
- 23,038
Leo jioni baada ya hekaheka za ziara ya viongozi wa ACT Wazalendo visiwani Zanzibar, nikaamua kupita kwenye kijwe kimoja maarufu hapa Kijitoupele.
Naikumbuka sehemu hii niliwahi kusikiliza hotuba ya komandoo mzee wetu Salmini Amour katika moja ya mikutano yake akiwa raisi alipoamua kuchekesha hadhira kwa kumzungumzia mzee mmoja maarufu aleitwa juma mapilau.
Hapa kuna jamaa mmoja huuza madafu na kwa kweli madafu yake huwa yamejaa khasa maji na ile minofu ya nazi, nikakumbuka kuhusu fedha za madafu yaani fedha za Kitanzania.
Nikamuuliza vipi aonaje mstakabali wa siasa za Zanzibar na uwepo wa Maalifu Seif, na Bernard Membe?
Akanijibu tu kwamba "Wanatimiza wajibu wao kama wanasiasa lakini hamna kitu CCM yashinda Zanzibar. Akaendelea akasema, "ni kama vile wanafunzi wametokea Assembly na waingia darasani na wakuta ubaoni kuna maswali upande mmoja na majibu upande mwingine".
Hii ikanikumbusha miaka ile ambayo kuna wakati mkoani Dar-es-Salaam wanafunzi walikuwa wajihaha kutafuta mitihani ya kununua na wakipewa mitihani feki wanakuja kufeli.
Lakini wale wanafunzi mahiri walokuwa wakihudhuria masomo ya ziada yaani Tuition ya walimu Njowoka na yule mwingine wa shule ya msingi ya Muhimbili wao walikuwa wametulia tu wakifanyia mazoezi maswali ambayo kumbe yalikuwa ndo majibu yenyewe tayari.
Anyway, nikamuuliza muuza madafu kwamba pamoja na kuuza madafu pia hujishughulisha na majukumu yapi? Akajibu akasema yeye kitaaam ni fundi wa kufunga ving'amuzi na televisheni majumbani na ujuzi huo aliupatia VETA na baadae mwaka 1995 akatimkia Uingereza baada ya machafuko.
Tukazungumzia sana Uingereza maana alinikumbusha maisha ya Uingereza ambako kwa kipindi fulani niliwahi kuishi miaka karibu 10 ilopita nikiwa katika harakati zangu barani Ulaya na Amerika.
Akasema alipokuwa Uimgereza hakupata nafasi ya kusoma sana kwani alikwenda kama mkimbizi na baada ya maisha kutomwendea uzuri aliamua kurudi nyumbani maana alimuacha mke na mtoto mmoja.
Muuza madafu huyu akaendelea kutoa somo la udiaspora na umuhimu wake kwa wale walioko Diaspora.
Akaendelea, "Diaspora wengi hawatambui kwamba serikali inawahitaji sana lakini wao hawataki kutumia "proper Channels" yaani njia maalum.
Wafanye lobbying kwenye sekta zote elimu, sayansi na teknolojia, kilimo na mengine mengi na serikali itawaunga mkono".
Akaendelea, "kwanza Watanzania wengi wamesoma tena katika vyuo vikuu vya maana tu lakini wengi wanafanya kazi za ujira wa kujitosheleza wao na wanakosa ziada yaani "disposable Income".
Watanzania hawa wengi wao kwa sasa ni wafuasi wa wapinzani hivyo hawana umoja wa kuwafanya wawe kitu kimoja na wawe wanafanya "lobbying" kwa serikali kwenye masuala mbalimbali".
Akasema "wengi wamejiiingiza katika uanaharakati zaidi kuliko kufanya bidii kutafuta fursa zilizoko Tanzania."
Akawasifu sana ndugu zetu wachaga akasema sasa hivi amesikia kuna baadhi ya wanawake wafanyabiashara wa kichaga wanasafirisha mbogamboga na baadhi ya vyakula mpaka magimbi kwenda huko Uingereza ambako kuna soko zuri sana.
Akasifia juhudi za rais Magufuli katika kujaribu kuweka nchi kwenye mstari unotakiwa lakin akasisitiza kwamba huyu raisi Magufuli yeye si kama JK kwai hana mizaha.
Akatoa ushauri kwamba madiaspoa wa kitanzania waige wenzao wayahudi ambao sasa hivi wameigeuza Israeli kuwa nchi kamili ya maziwa na asali.
Hapo mimi sikuweza kukubaliana nae nikamkumbusha kwamba Israeli inakalia sehemu isio yake kwa mabavu tangu mwaka 1948.
Muuza madafu huyu akasema " ni sawa lakini mimi nashauri sana kwenye kufanya "lobbying" khasa kwenye mabalozi yetu huko."
Akaendelea, "we umesikia tena kuhusu matawi ya CCM Ughaibuni au matawi ya Chadema Ughaibuni yakifanya mikutano?
Hata ile mikutano ya wao kwa wao imekufa kabisa maana ama hamna ari au wamekosa matumaini kabisa.
Ila watanzania wa diaspora wakiendelelea kushiriki kuinanga serikali ambayo walikuwa wanaihitaji eti tu kwasababu hawampendi raisi alieko madarakani basi wanazidi kujiharibia na kuonekana wao hawahitajiki"
Ni lazima wakumbuke wao na familia zao walizo nazo huko ughaibuini na mstakabali wa maisha yao ya baadae ama wakiwa hukohuko ughaibuni au wakirudi Tanzania "akamaliza.
Baada ya kauli yake hii ya mwisho nami nilikuwa ndo nimemaliza dafu langu na akanifanya nimkumbuke mwosha viatu.
Nikasema kweli usiwadharau wauza madafu na maembe au wakokota mikokoteni ambao wengine wana familia zao na wanaishi maisha ya kawaida kabisa.
Ila ujumbe ndo huo wana diaspora inabidi muanze kutafakari upya mwelekeo wa jitihada zenu mitandaoni na ikibidi kugeuza mwelekeo huo huo uwe wenye kujisogeza karibu na serikali badala ya kuzidi kujitenga nayo.
Nikakumbuka kuanzishwa idara ya diaspora ofisi ya waziri mkuu lakini nilisikia yule dada yenu ambaye ndiye aliekuwa awe kiunganishi aliamua kuachana na mambo ya udiaspora na sasa anaendela na maisha mengine.
Ni hayo tu ndugu zangu.
Mimi ndo nikapanda Vespa yangu kwenda "home" Mwanakwerekwe.