Mzalendo2015
JF-Expert Member
- Aug 14, 2012
- 6,710
- 9,063
Kwenyu waheshimiwa sana Uhuru Kenyatta na William Ruto, bado siku 3 tu kufikia siku ya Uchaguzi wa marudio.
Ushauri wangu wa mwisho ni kwamba Uchaguzi huu wa marudio unaweza kuipeleka Kenya kwenye vurugu kama za mwaka 2007...!Kila dalili inaonesha hivo na hakuna kitakachozuia.
Maombi ya kiroho na Polisi hawataweza kuzuia machafuko yakayotokea siku ya tarehe 26 Oktoba 2017.
Kama mtalazimisha Jubilee wapige kura au kuwazuia NASA wasiandamane itakuwa ni kuongeza petroli kwa moto...!!.Marudio ya Uchaguzi huu yametokana na Mahakama ya Kenya kufuta matokeo ya taehe 8/8/2017 baada ya kuoneka kulikuwa na udanganyifu mkubwa na wizi wa kura.
Baada ya uamzi awa Mahakama, NASA walipendekeza makamishna na Mkurugenzi Chiloba waondoshwe kwenye Tume ya IEBC lakini hakuna aliyekubali kuondoka.
Jubilee mkiwa ndo wasimamizi wa Serikali kwa sasa mmeshindwa kusimamia zoezi la kuwaondosha wafanyakazi wa Tume waliotuhumiwa kujihusisha na kughushi matokeo..
Lakini kama hiylo halitoshi Jubilee mmeshiriki kukuza mgogoro kwa kuandaa mabadiliko ya sheria za Uchgauzi zitakazo tumika kwenye Uchaguzi wa marudio kitu ambacho hakiko sawa.
Wafula Chebukati hajui afanyeje maana yuko kwenye cross-roads. Ezra Chiloba keshakimbia kwenda likizo anaona mambo ni magumu. Wafula hajui achagua njia ipi ya kupita maana hajui kama uchaguzi ufanyike au usifanyike kwa hali ilivyo tete.....!!
Mgombea Urais wa NASA Raila ameshajitoa kwenye kinyang'anyiro na kesha waambia wafuasi wake waandamane siku ya Uchaguzi badala ya kupiga kura. Hii ni picha inayo ashiria hali ya hatari. Fikiria chama pinzani wanaandamana na chama tawala wanapiga kuta, nini kitatokea..?? Lazima yatokee mapambano na madhara yake yatakuwa ni makubwa. Polisi hawataweza kudhibiti umati huo kwa nchi nzima..!!
Kama Kenya ni yenu nyote kwa maana si ya Uhuru wala ya Ruto, si ya Jubilee wala , si ya Kalonzo na wala si ya NASA...basi kubalianeni kufuta Uchaguzi huo mkae chini nyote, Jubilee, NASA, IEBC ili mfikie mwafaka. Vinginezo mnarudia hali ya mwaka 2007 ya kutaka kurudi Ikulu kwa kumwaga damu za Wakenya.
Mungu ibariki Kenya!