Ushauri wa ujasiriamali, sina uwezo mzuri kimasomo

be unique

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2016
Posts
2,381
Reaction score
2,287
Habari zenu wanaJF,

Kama kichwa kinavyojieleza hapo, mimi ni kijana mdogo nina kama miaka 22 nimefanikiwa kusoma mpaka cert ya procurement & supply.

Lakini katika kusoma kwangu nimesoma kwa shida sana sina maana kwamba ada haikupatikana la hasha bali ni uwezo wangu kimasomo sio mzuri kufaulu mpka nitumie nguvu ya ziada.

Ushauri wangu hapa ni kwamba nikisema niendelee na diploma natakiwa kusoma masomo ya nabe ambayo ni mwaka mzima hli kuweka cheti changu sawa na hapo bado naweza nikafeli.

Kitu ambacho nilitaka kuomba ushauri ni kwamba nimefikiria kujiusisha na biashara maana mtaji naona sio shida kwa sababu ndugu zangu ni watu wenye uwezo wastan ambao hawashindwi kunisaidia maana nimeona shule kama namalza ada za wazazi bila sababu maalumu.

Natanguliza shukran naomba ushauri kwa hili.
 
Huu Uzi Ni vema ukapelekwa jukwaa la biashara na uchumi na ujasiriamali. Pia mkuu, ukienda pale pana mada nyingi sana ambazo zimeshajadiliwa kuhusu biashara za aina mbalimbali. Na pia zimejadiliwa kwa watu wenye mitaji tofauti tofauti..

Nadhani ukiingia utapata mwanga Wa kutosha kuhusu biashara kiujumla. Vivyo hivyo jukwaa la kilimo na ufugaji pia kuna mambo mengi ya kujufunza pale. Vinginevyo...

Ni vema kama umetambua kuwa hujiwezi kwenye masomo na Ni vizuri kufanya kile unachokipenda.
 
Khasante sana kwa ushauri wako.
 
Ww unaish wapi Una hobi Na kufany nn ktk maish yako Na unahsi icho unachotqk kufany unadhan mtaj wake Ni kuanzia kiss gan
 
Kama kichwa panzi bora uache tu kusoma. Maana kusoma pia kipaji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…