Ushauri wako ni muhimu katika hili


Majibu yako hapo juu yanaonyesha bado hujafanya utafiti wa kutosha na pia huna experience ya kilimo.
Maadam umeomba ushauri, mimi ushauri wangu nitakupa sambamba na namba zako hapo juu:
1) Usichague tu zao la kulima maadam umesikia kuwa zao hilo linalipa. Badala yake nenda kwenye shamba la mtu aliyefanikiwa katika zao fulani halafu ukajifunze kivitendo.

2) Fanya umoja na mtu ambae ana ujuzi wa kilimo zaidi yako

3) Hili ni muhimu sana. Lijue soko lako ama sivyo utavuna mazao ukose pa kuuzia.

4) Sababu aliyokupa Mzee wako ni ya kiuhalisia.Amekushauri kutokana na hali halisi. Pia kwa vile mtaji ni wa kwake itabidi umsikilize. Kama utapenda ku-take risk kwenye kilimo hapo baadaye basi fanya hivyo kwa pesa yako na sio pesa ya mtu mwingine!
 
Nimekuelewa Sana mkuu shukrani saana mungu akubariki saana [emoji120]
 
Fanya ambacho una uzoefu nacho na unauhakika wa soko.

Kama umeamua shirikiana na mwezako ni heri mngeshirikiana katika ufugaji huo wa kuku tena kwa wote kuwa na michango sawa ( kila mtu atoe mil. 2) au katika mlingano mwingine.

Kilimo anachotaka hata uzoefu nacho naona huna lakini hujui soko lake baada ya uvunaji na pia kilimo kinaweza feli kulingana na hali ya hewa.

Ushauri wangu:

FANYA UFUGAJI WA KUKU.
Mzee wako kakupa mtaji ili ufanye huo ufugaji hata kama ukianguka atakuwa na wewe kukusaidia kuliko huko unakotaka kwenda kwa Jamaa yako ambaye yeye ana mtaji Mdogo.

Hata baada ya kupata faida hakika timbwili litatokea lazima atataka mgawane faida sawa...... Sisi binadamu tuna tamaa hata kama kila mmoja mlikubaliana atapata faida kulingana na asilimia ya mtaji alioweka katika hiyo biashara.

HITIMISHO:

FUGA KUKU, FUGA KUKU.
 
Usilime vitunguu mkuu

Aaah nikisikia hii kitu kichwa kinataka kupasuka.
Bora ulime mboga mboga za miezi mitatu na ambazo zinapiga round kuvunwa
Yaani unachuma zaidi ya mara moja.
 
Usilime vitunguu mkuu

Aaah nikisikia hii kitu kichwa kinataka kupasuka.
Bora ulime mboga mboga za miezi mitatu na ambazo zinapiga round kuvunwa
Yaani unachuma zaidi ya mara moja.
Nimekuelewa,inaelekea ulisha wahi kujaaribu?
 
Sawa mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…