Ushauri Wako Ni Muhimu Tafadhali!

SSJ

Member
Joined
Oct 10, 2018
Posts
15
Reaction score
5
Nianze kwa kuwasalimu nyote humu JF..Hakika JF ni kisima cha maarifa ambapo wote twajifunza vitu vingi humu,kwakufahamu hilo ndio sababu ya mimi Kuandika yangu machache siku ya leo

Ulimwengu wa biashara unakua kwa kasi kila leo na hii huchochea uanzishwaji wa biashara hizo,miradi na mengineyo ili kuendana na kasi hiyo inayozungumziwa,na kiukweli biashara ndizo zitazoendesha maisha ya kila siku ya watu haijalishi biashara hyo ni kubwa au ndogo!

Mataifa mengi ulimwenguni siku zote huamasisha hasa vijana kuweza kujiajiri na kufanya kazi kwa bidii ili kujenga na kuboresha maisha yao ya sasa na hata baadae..Kwa kulifahamu hilo mimi Kijana wa kitanzania(miaka 21) nimekaa na kuwaza katika kuwashirikisha wana JF wenzangu katika hili ninalokwenda kulieleza..

Napenda mafanikio!,yani nayapenda..Kuna mtu mmoja ambaye nilifahamiana nae hapo nyuma katika hizi semina za maendeleo na ujasiriamali na baadae tukazidi kuwa na mawasiliano,ni mtu na biashara zake na maisha yanayoeleweka kabsa!..Niliwahi kumtafuta hapo nyuma ili kuzungumza nae mawili matatu ila alikua ''bize" sanaa..Week mbili nyuma ndipo alikubali tuonane..Nilihitaji kuongea nae vingi ila moja ya hayo ni yeye kunisaidia connection au yeye mwenyew kunipatia kazi kama ipo..

Baada ya siku mbili za mazungumzo yetu alinitafuta na bila kupoteza muda alianza kunipa majukumu mbalimbali kwenye baadhi ya shughuli zake,kuanzia hiyo siku mpaka leo niko nae..Kazi zake nazifanya vizurii..Ila juzi Alinambia ni vizuri nikampelekea wazo la biashara(Business Idea) ambalo naamini naweza kulifanyia kazi ili nisiwe tena mfanyakazi wake bali tuwe business partners na biashara niisimamie ila mwisho wa mwezi tunagawana nae faida bila kuathiri mtaji..

Alichonambia ni kwamba kwake mtaji sio kitu cha kuwaza sana bali nimpelekee business idea ili ifanyiwe kazi..Binafsi nimekaa na kufikiria nikaona pamoja na kutoniwekea limit ya mtaji ni vzuri pia nikamweleza biashara isiyo na mtaji mkubwa sana na istoshe bado sina uzoefu katika ulimwengu wa kibiashara..

Yafuatayo ni Mambo/Njia kuu Sita rahisi nilizotumia katika kupata wazo la biashara[emoji419]

1..Kupitia kusoma baadhi ya vitabu
2..Kupitia marafiki na mazungumzo
3..kupitia familia
4..kupitia kutatua kero za kwenye jamii
5..Kupitia Mambo Unayoyapenda
6..Kusafiri

Katika yote hayo nimeangukia katika namba 5,yani kitu ninachokipenda,yani utanashati/urembo na vifananavyo na hvyo..Kwa kifupi nimefikiri ni bora kufungua frame ama duka kwaajili ya uuzaji wa nguo na viatu,na hilo ndo wazo langu!! nimeegemea huko kwakua ndo kitu ninachokipenda na nitakifanya kwa moyo

Tayari nimeshamueleza muhusika wazo langu na amelikubali tayari ila alichoniambia niandae na nimpelekee Business plan na vitu vya muhimu katika biashara hyo then mengine yaendelee..Maswali yangu ninayohtaji msaada wenu ni machache..
_Mtaji wa kuanza hii biashara yaweza kuwa bei gani hata kwa kukadiria?

_Ipi ni Location nzuri kufanyia biashara hii kwa Dareslaam?

_Bidhaa husika huwa zinapatikana wapi hasa kwa rejareja?

_Mbinu bora za kimauzo na kimasoko ni zipi?

_Ipi ni namna bora ya usimamizi wa hii biashara?..maana mimi sio mzoefu

_Biashara hii ina hali gani kwa sasa kwenye soko?

_Faida/ubora na changamoto zake ni zipi?

Tony Robins Aliwahi kusema:"Kuna Nguvu Kuu Sana Ya Mafanikio Ndani Ya Kila binaadamu,Ambayo Ikiamshwa,inaweza Kuwezesha Kufanikiwa Kwa kila Maono ,Ndoto,Au Matamanio Na Kufanya Yawe Halisi..

Karibuni Wakuu!








Sent from my SM-J110H using JamiiForums mobile app
 
Sikukatishi Tamaa ila biashara ya duka ni ngumu sana ukizingatia mtaji sio wako ni wa mtu anataka faida kwa kukushauri ningependa uanzishe kampuni, hata kama itadeal na urembo na utana shati kama unavyopenda inawezekana kwa mfano kama upo dar es salaam kuna watu wako mikoani unaweza buni mbinu kupitia kampuni yako kuwapelekea mzigo uko na wanakulipa cash au cheque sana sana ukatengeneza network ya kujitangaza wewe kazi yako kuchukua mzigo kariakoo au kuagiza china au njee na kuwapelekea popote walipo mikoani sasa hv technolojia imekua unaweza ukaingia online na kuchek bei na kuona wewe utapata faida vipi? .

unaweza pia anzisha kampuni inayojiusisha na mambo ya mitindo kuvalisha bibi harusi,bwana harusi,kupamba kumbi za harusi kuwa na brand yako ya ku design mavazi na mitindo inawezekana ila kazi hii uifanye kwenye mfumo wa kampuni ndio faida itaiona sio mfumo wa duka .

pesa ya sasa ipo kwenye tender sio duka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…