Ushauri wako ni upi? Hamornize abaki WCB au aondoke?

kada maarufu

Senior Member
Joined
Jun 14, 2017
Posts
149
Reaction score
82
Pamekuepo na taarifa za mara kwa mara za mmoja wa wanamuziki wa WCB Harmonise kuondoka au kutaka kuondoka katika lebel yake hiyo iliyomtoa na kukuza.

Binafsi baada ya kusoma mijadala mingi uko kwengine nimekua na mixed feeling kuhusu hilo, kiasi hata sasa uliniuliza kipi naona bora sitakua na jibu sahihi.

Kwaajili ya maendeleo ya sanaa yetu embu wadau tushauriane kipi bora kwa Harmonize kwa sasa na Kwasababu gani, labda licha ya kuwa mimi pia nitapata uelewa ila labda hata yeye au uongozi wake utapita hapa na kuchambua mawazo.

Nawasilisha
 
Sisi haituhusu pambana na hali yako cos wewe ndo unaweza kujenga career yako lakini pia wewemwenyewe unaweza kuaribu career yako kwa siku moja tu so kazi ni kwako kusuka au kunyoa
 
Harmonize usipoteze muda kama umeona ni vyema kuondoka na umekuwa mkubwa na sasa unaweza simama peke yako wewe nenda!

Lakini hakikisha unatokea kwenye mlango ulio ingilia!

Wewe nenda lakini hatuhitaji kusikia maneno oooh nafanyiwa figisu oooh nawindwa oooh nalogwa.....
 
Aondoke au abaki mi sinufaiki na chochote...kwahiyo ni yeye tu...
 
Advertise ya kwanza umeshindwa kupata USA visa on time ukakosa show kitu ambacho haujawahi kuki'experience hivyo ujue ukiwa solo ile easy flow uliyokuwa umeizoea hatakuwepo tena, 75% ya fans wako ni kwa sababu uko WCB hivyo ujipange kutengeneza fans wako, jiandae kwa figisu kwenye adverts, endorsements na shows. Uphill task ahead kijana, usipojiangalia utayakumbuka maneno ya Master J pale Bongo Star Search na utaanza kuyaamini.
Uamuzi ni wako kusuka au kunyoa though sometimes ni vizuri kutokuwa muoga na kuchukua maamuzi magumu, maybe utaweza and you gonna prove us wrong.
Nilisema Rich Mavoko atapotea jumla kuna waliodai akitoka WCB ndipo atamzidi Diamond sasa yuko level na Timbulo where he rightly belong.
 
Muziki ni pesa,na ili ukunufaishe unatakiwa uwekeze pesa;bila kuwekeza pesa nyimbo zako hazitavuma hata kama unakipaji kumzidi muumba.
 
Mamake akitoka pale Wcb ata ile mbunye ya yule demu ake chinyenya ata ona utamu ake!
 
Tatizo kubwa nionalo ni pesa inaonesha mkataba unambana sana au hafaidiki
 
Aondoke abaki sisi inatusaidia nini??
 
Mimi nimshauri tu hamornize tulia hapo hapo kwa diamond utajuta ukitoa mguu hizo cheni utaziuza mwenyewe.. HAMONIZEkuna vitu viwili tu vikikuondokea unae da Luisa maji ya viroba!! moja Sara yule mzungu pili diamond ukifunga mlengo kwa mond figisu za bongo flab’s huziwezi!! bakia kwa mondi.. Diamond ndio pekee aliezishinda fitna za bongo hadi leo anavaa macheni ya milioni 150.. hivo timu yako uliyonayo watu wanategemea utoke ndio wale.. acha ujinga watakucheka watu!!
 
Tatizo kubwa nionalo ni pesa inaonesha mkataba unambana sana au hafaidiki
Hili linawezekana, tatizo ni kwamba kipindi anasign ule mkataba alikuwa nobody, si unajua underground akiwa na njaa ya kutoka ukimletea mkataba wowote mezani anasign tu hata kama amepewa 5%, akishapata jina ndo anaanza kutambua kwamba mkataba ulikuwa wrong. Nafikiri ndio situation aliyonayo sahivi, anaona anapata show za pesa nyingi ila yeye hanufaiki kivile, ila ni bora ahangaike kukaa mezani kurekebisha mkataba kuliko kufikiria kuondoka
 
Mjuwe WCB Wana TV na Radio kumtangaza karibu Africa yote. Kupitia DStv Azam. SratTimes. Akiondoka biashara yake itafifia Sana. Biashara NI matangazo ya kisasa. Tujiulize kwa niniamekosa VISA ya kwenda USA?
 
Mjuwe WCB Wana TV na Radio kumtangaza karibu Africa yote. Kupitia DStv Azam. SratTimes. Akiondoka biashara yake itafifia Sana. Biashara NI matangazo ya kisasa. Tujiulize kwa niniamekosa VISA ya kwenda USA?
Ndo kitachotokea hiko.
 
Baada ya kusikiliza majibu ya Salam kuhusu nyumba ya ray van na mboso binafsi nakubaliana kabisa na harmonize kujiondoa hapo wasafi!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…