Ushauri wako please!!!!!!!

ufumawicha

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2014
Posts
504
Reaction score
209
Nina genge na kaduka kadogo nyuma yake.Tatizo wenye maduka makubwa wanaonizunguka wamekuwa na kawaida ya kuja kuangalia vitu ninavyouza mpaka ninaogopa hasa ikichukuliwa ni mwezi tu nimeanza nazi hii na istoshe wao wana mitaji mikubwa sana.Wakati mwingine wanakuja eti kununua viberiti wakati na wao wanaviuza!Nishaurini wadau hali hiyo ni kawaida au kuna ajenda nyingine?
 
Maji ukiyavulia nguo. ........
 
Wasiwasi wako unakufanya usijiamini na kupelekea kuwaza mabaya ambayo yanakutia hofu.
Piga kazi na usiangalie sura ya mtu aiseeee......
Pengine wao pia wanakuogopa kwa kutaka kujua kinacho kufanya wewe na mtaji wako mdogo uamue kuweka kibiashara chako kwati yao pamoja na kwamba wana mitaji mikubwa.
Muombe Mungu akufanyie wepesi na uweze kuyashinda majaribu.
 
Ushimen
Asante sana kwa ushauri nadhani ni hofu tu!
 
Kwani hukujua kwamba biashara INA mengi!! Kama ulijua tulia piga kazi nafkir ushajua nn wanamaanisha
 
kazi yako ni kuuza tu ndomana ulileta bidhaa ziuzwe, hata akija rais jpm muuzie si ndo kazi yako?
 

We nenda tu huko kwa mganga unakowaza ukaliwe pesa yako yote ya mtaji maana badala ya kuwaza kununua na kuuza unawaza kwenda kumpa pesa yako mganga ..hopeless
 
Komaaaaa.....hizo ndo changamoto zenyew kamwe ucteterek bak njia kuu n songa mbele
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…