Hii misimamo hii...
Kuna mdada nikiwa mdogo alikuwa gumzo la mitaani... Yeye alikuwa mlokole...miaka hiyo ya 80s walokole walikuwa wachace sana sehemu tunapoishi na tulikuwa tunawahita kanisa la "kulia" kwa kuwa walikuwa wakisali wanalia.
Huyu dada alikuwa amefikia umri wa kuolewa, lakini cha kushangaza ni kuwa kila mwanaume alokuwa anamtokea yeye alikuwa anakemea...yani atakusalia barabarani mpaka utoke dima kwa aibu.
Miaka ikakatika akaanza kuzeeka...tukasikia ameacha ulokole...nadhani aligundua wanaume wameanza kumuogopa maana mimi nilikuwa mtoto lakini nilikuwa najua stori zake za ubingwa wa kukemea wanaume "mapepo. Lol"
Mpaka nimekuwa, nikaenda boarding school alikuwa hajaolewa...
Hivyo wadada wawe makini na dini...extremism hai work kwenye kutafuta life partner. Kuna watakaokuja kwa gia ya ndoa na kubadili dini lakini mwisho wa siku wakipata wanachotaka wana ku dump