Ushauri: Walimu wapitishwe Sekretarieti ya Ajira kama kada zingine

Ushauri: Walimu wapitishwe Sekretarieti ya Ajira kama kada zingine

Midimay

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2015
Posts
3,036
Reaction score
5,039
Huu utaratibu wa kuwaambia watu kuomba ajira kisa tu wamesoma na wamemaliza ngazi zao elimu sio sawa, na umeshapitwa na wakati hapa nchini. Na uchumi hauna tena uwezo wa ku-accomodate majority ya walimu na hata kada za afya.

Njia pekee ambayo itaisaidia kwa asilimia kubwa utapeli, rushwa katika mchakato, undugunization, ukabilization, ufahaminization nk katika mchakato huu ni kuwapitisha kwenye interview za sekretariat ya ajira au tume huru yoyote.

Mchakato usitishwe au wote walioomba waitwe kwenye mchakato wa usaili wa aina 3:
  • Usaili wa kuandika awamu ya 1
  • Usaili wa kuandika awamu ya 2 (hii pia huitwa michujo)
  • Na usaili wa ana kwa ana na panel
Hakuna namna nyingine fair sorting zaidi ya hiyo.

Suala la kujitolea pia siku hizi imekuwa ni opportunity na sio fair pia. Lina figisu zote kama ilivyo ajira.

Wizara ikisema inawachukua waliwahi kujitolea, jua hapo waziri ameingizwa kingi na vi-cartels vya wizara yale. Wamempotosha makusudi ili wanufaike na mchakato. Ama sivyo basi wamewaza kidogo sana. Wawaze tena.

Waziri Ummy, omba bajeti ya dharura ya kufanyia interview ili upate walimu wa uhakika. Mtakuja hapa kunishukuru.

Ukitaka kuamini, utafiti ufanyike kati ya ubora wa watumishi wanaopitia usaili wa sekretarieti na zile ngoma ambazo zenyewe zinaunga moja kwa moja.

Mtaona tofauti kubwa.

Ni hivyo tu yani.
 
Katibu mkuu utumishi wiki hii yupo Mkoani kwetu.

Na kapita halmashauri kwetu na Hili kaliomgelea.

Kasema; Kwenye kufanya application hizo ulizotaja UZOEFU hautakua moja ya vigezo kwasababu, ukiruhusu UZOEFU liwe ndio sababu ya kupata nafasi then, itakua umeruhusu vingi.

Alichosema wenye uzoefu na wasio na uzoefu wotee watakutana kwenye USAHILI.

Aliyebora zaidi ndio atachukuliwa.

#YNWA
 
Back
Top Bottom