platozoom
JF-Expert Member
- Jan 24, 2012
- 9,424
- 11,320
Naipongeza Serikali kwa kuja na mpango wa Bima ya afya kwa wote.
Pamoja na kuwa na wazo zuri lakini utekelezaji kama jambo lolote kubwa utakuwa na changamoto. Na moja ya changamoto yake ni kiwango cha fedha kwa kwa mchangiaji mwenye familia kwa kuzingatia hali halisi ya kipato. Kutokana na ukweli kuwa kila mtumishi wa wa Serikali anachangia mfuko wa NHIF, Serikali kwa sasa inalenga kundi kubwa ambalo lipo nje ya Serikali.
Kwa sasa, ukiondoa Watumishi wa Serikali, kuna Watumishi wa sekta binafsi ambao kupitia kwa Waaajiri wao wameungwa katika mfuko wa NHIF kwa mfano CRDB. Lakini kuna kundi dogo kutoka katika baadhi ya Sekta binafsi hasa makampuni makubwa na mashirika ya Kimataifa wao wapo katika makampuni binafsi ya bima (ambayo ni ukweli kuwa wao wana mikataba na hospitali chache za mjini na nyingi zikiwa kuanzia ngazi ya kituo cha afya).
Nilikuwa naishauri Serikali, kwa kuwa kuna Wafanyakazi wengi wa Sekta binafsi ambao ni wanachama wa NSSF (Mfuko wa pensheni) na ambao hawapo katika mfuko wowote wa bima ya afya na wao kujumuishwa katika mfuko wa Taifa wa bima ya afya (NHIF). Kwa sasa wanachama wa NSSF wanapata benefit ya huduma za matibabu lakini ikiwa na limit sana tofauti na wanachama wa NHIF.
1. Kwa mfano, mwanachama atapata huduma kutoka katika kituo kimoja tu alichoandikishwa
2. Gharama kwa siku kwa mteja mmoja haitakiwi kuzidi shilingi 40,000. Kwa mfano gharama tu ya consultation ni 5000 kwa vituo vingi, hapo bado vipimo na na dawa.
Kwa hilo hapo juu, napendekeza kwa kuwa NSSF inachukua fedha za Wanachama mpaka pale wanapostaafu, basi hiyo benefit ya matibabu waipeleke NHIF ili wanachama wao waweze kupata huduma kama wanachama wengine wa NHIF.
Nadokeza tu, Wafanyakazi wa NSSF wao ni wanachama wa NHIF! Wanapata huduma kwa kutumia kadi za NHIF na si NSSF!