Ushauri wangu: Diamond, Alikiba na Harmonize wafanye "show" ya pamoja ili kufanikisha mchango wa matibabu ya Joseph Haule

Ushauri wangu: Diamond, Alikiba na Harmonize wafanye "show" ya pamoja ili kufanikisha mchango wa matibabu ya Joseph Haule

Mc PIPI

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2020
Posts
325
Reaction score
442
Naam,hayawi hayawi yaweza kuwa.

Katika suala la mshikamano katika jambo Fulani basi tofauti huwekwa pembeni na kuungana pamoja kutekeleza Hilo jambo kilolo mbele yenu.

Tangu taarifa za kuumwa kwa legend P Jay zitoke nimeshuhudia maelfu ya watu wameguswa mno na taarifa hizo mpaka kufikia hatua ya kuhamasishana kuchangia matibabu.

Ni jambo zuri kwa wazo Hilo NAMI nimekuja kutia Neno la kuunga mkono Hoja na kujazia Nyama.

Kwa heshima kubwa aliyojijengea huyu mheshimiwa kwa umma wa watanzania wakiwemo wasanii.Nina hakika kubwa kuwa hakuna msanii asiyemheshimu huyu jamaa.Sasa kwa msingi huo ni muda mwafaka sasa enyi wasanii wa bongofleva mkiungana na niliowataja hapo juu kufanya show kubwa ya pamoja kwa ajili ya kuchangia matibabu ya huyo jamaa.

Na Nina uhakika endapo katika show hiyo watajwa hapo juu mkajumuika pamoja basi kama ni kwa Mkapa,Sokoine,Samora,Sheikh Abeid,CCM Kirumba,Mkwakwani na Jamhuri. Nina uhakika mtajaza na hivyo mkawa mmetimiza WAJIBU wenu na kuliko kusubiri vinginevyo Ili muanze kuungana kumwimbia nyimbo na show offs zenu ambazo hazifai.

Ewe msomaji kama Neno Hili limekukolea ungana NAMI kupaza sauti hii Ili iwafikie hao watajwa.

1644569544872.png
 
Wabongo mnapenda michangomichango
Kwani hamuwezi kufanya michango kimyakimya
Au ndiyo michango inageuzwa fursa kama kawaida yenu

Ova
 
Back
Top Bottom