Ushauri wangu juu ya kodi na TRA

Nyumbalao

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2014
Posts
494
Reaction score
522
Baada ya kuwasikiliza wafanyabiashara na matokeo hata ya kubadilishwa kwa Mkuu wa TRA naona nami nitoe yangu machache ambayo yanaweza kuangaliwa kwenye bajeti ya mwaka huu au hata ya miaka ijayo.
1. Tatizo la uelewa bado ni kubwa mno kunatakiwa kuwe na juhudi za kimkakati za kuwaelewesha wafanya biashara wetu juu ya maswala mazima ya kodi na kanuni zetu ili watu waelewe jinsi ya kuenenda nimekuwa nikijitahidi kutoa elimu humu ya https://www.jamiiforums.com/threads/mambo-muhimu-ya-kuzingatia-katika-uendeshaji-wa-kampuni kwa kutumia thread hiyo tu na maswali ninayojibu PM nimejua kuwa tunahitahitaji elimu kwa wafanyabiashara kuhusu kodi
2. Swala la kuongezeka mapato ya serikali wakati biashara zinafungwa nalo ni jambo zito ambalo maelezo yake kidogo ni magumu ila kihasibu hili linawezekana tu ikiwa watu walirudikiwa madeni na hivyo kuibidi kukubali. Na mtu anapokubali deni basi tuna debit (Deni) Account receivable tuna credit Mauzo(Revenue). Ushauri wangu kwa kuwa mkuu anapenda kuona mabilionaire wakiibuka ni wakati sasa kuwa na huruma kama alivyokuwa na huruma ya kufuta penati mwaka jana tunaomba kuangalia madeni yalioyo na zaidi ya miaka 3 ambayo kwa ukweli mchungu hayalipiki yafutwe kwenye vitabu vya TRA tuanze upya
3. Tatizo la Tax audit nafikiri uliwasikia wafanya biashara wakilalamika kuwa wamepeleka hesabu zao halafu tena wanakuja kulipa tena kodi kubwa. Hili kwanza imetokana na tofauti kati ya uhasibu wa kufunga hesabu na Uhasibu wa Kikodi hili ni swala la kitaalamu kidogo lakini shida tuliyonayo hapa kwetu hizi tax audit mtu zinachelewa kufanyika mno ambazo mara nyingi hawa wakuu wakija mtu amefanya makosa mengi ya kikodi na hivyo kukutwa na kulazimika kulipa kodi kubwa. Ushauri wangu najua sheria inawaruhusu TRA kufanya Income tax audit ya miaka 4 na kodi nyingine hazina time bar lakini ni ukweli kuwa tax audit nyingi zinaishia kuwaumiza wafanyabiashara hasa wa kati basi tujitahidi tuwe tunawafanyia wafanyabiashara hizo tax audit kila mwaka ila ikishindikana kila baada ya miaka miwili especially wale ambao tunaona kunaweza kuwa na impact kwenye swala zima la kodi ya nyongeza. Nyingine ni kufanya desk review ya returns zote na kuwapa feedback kwamba kuna kodi hizi kwa hesabu hizi ulipaswa kulipa wewe ujalipa. Mfano withholding tax on rent, SDL na PAYE yaani hizi hazitakiwi eti mpaka mtu afanyiwe tax audit 4 years zinarudikana na fine za kutosha wakati ambapo TRA ingepokea nakufanya desk review na ambazo ziko wazi wapewe assessment walipe. Tatizo lingine kubwa hapa kwenye TAX AUDIT NI ule ubabe wa kuadd back matumizi halali ya biashara ili wapate kodi kwa kulazimisha hii sijui dawa yake ni nini lakini ni vyema ikatafutwe afisa anaamua tu kukubali asilimia 20% ya matumizi kama ndio halali kwa biashara.
Nawasilisha
 
Kwa kweli Budget hii imeonyesha kwa ukweli jinsi serikali ilivyoadhimia kuweka vizuri mazingira ya biashara tupambane kuzalisha kwa hizi Tozo zilizoondolewa hakika tutakaa vyema. Hakika SERIKALI imekuwa sikivu. Ukitaka kuona mambo yenye uzito kwa haraka pitia fungu kuanzia 37 mpaka 52. Karibu
 

Attachments

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…