Chance ndoto
JF-Expert Member
- Mar 8, 2017
- 4,363
- 10,265
Maoni yangu tu kwa serikali na nchi yangu pendwa Tanzania.
Kumekua na Sintofahamu kubwa sana haswa kwa vijana wanaokesha mitandaoni, au watanzania wanaotumia mitandao. Kuna uhuru mkubwa sana wa Mitandao sasa, ambao ni safi kabisa. Ila siintofahamu zimekua nyingi saana.
Leo huyu kakamatwa, kesho huyu katekwa. Kesho yule kabakwa, ila vijana au watu wanaotumia mitandao wanapata jazba, taarifa zinachagizwa na chuki, kutukanana mitandaoni, watu mitandaoni wamekua na hasira sana. Hii inapelekea hata wasiofahamu habari vizuri, kuongelea vibaya zaidi kuhusu habari hizo. Juu yake zinakuja movement against serikali iliyo madarakani.
Nayo serikali inatakiwa itoe neno. Ikitoa neno linaonekana limechagizwa na movement ya mtandaoni, yaani hamna zuri la serikali wala mihimili yake. Nashauri, serikali itoe neno kwa mambo haya, Haswa Raisi wa nchi, X au JF ni ndogo sana, ila inaweza fikisha ujumbe mzito saaana kwa watu wasio mitandaoni.
Leo mtoto akipotea baasi ni serikali, Mtu akichinjwa serikali, msemaji akikosea herufi kuandika kwenye pdf. Serikali ya hovyo, Raisi akipita na gari zake nyingi serikali ya hovyo. Serikali imekua inatupiwa lawama zote.
Okay, leo imebidi niendelee kuandika, jana niliishia kaitkati. Raisi wangu Samia Suluhu. Ingekupendeza ungeongea na kamati yako ya ulinzi isikamate hawa vijana wa bavicha, waache waendelea na tamasha lao la vijana. Vijana wa chadema, inge wapendeza, mngeacha siasa za fujo na kukomoa , fanyeni tamasha lenu kwa amani.
Viongozi wa chadema, mimi naamini ipo siku chama chenu kikiwa na itikadi safi,mtatuongozea watoto wetu, wajukuu au sisi wenyewe. Siasa za kukomoa ningeshauri ziachwe na mshiriki kuijenga nchi kwa amani, inawezekana mko sahihi, ila hamko sahihi kwa utawala wa nchi yetu, Kwa vijana wakitanzania Haswa mitandaoni, ningependa muwe watu wa amani, tusishadadie kila kitu, bali tuijenge chi yetu, yawezekana sisi ndio viongozi wa baadae.
Asante. Nakosa maaneno maazuri na utulivu wa kuandika ila naiombea amani Tanzania, na furaha miongoni mwa wananchi wote. Bila tofauti zetu.