Ushauri wangu kwa BoT kuhusiana na upotevu wa Sarafu za Sh 500, 200, 100 na 50

Ushauri wangu kwa BoT kuhusiana na upotevu wa Sarafu za Sh 500, 200, 100 na 50

Mr Why

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2019
Posts
2,235
Reaction score
4,252
Kumekuwa na uhaba mkubwa wa Sarafu za sh 500, 200, 100 na 50 pasipo kupatikana mwafaka wa usumbufu huu

Ukweli ni kuwa sarafu hizi zinaibiwa na Wachina kupitia Mashine za kamari zilizotapakaa kila kona ya nchi hasa sehemu za starehe

Huwa Sarafu hizi zinaibiwa kwa lengo la kwenda kuyeyusha ili kujipatia vito nakadhalika

Jinsi ya kuondoa tatizo hili sio kutengeneza Sarafu nyingine bali BoT inatakiwa kusitisha uzalishaji wa Sarafu na kuunda noti ambazo hazitaibiwa tena na kwenda kuyeyushwa kama inavyofanyika kwenye Sarafu
 
Mkuu, chanzo ni holding ya hizo pesa,
Mfano mm binafsi nina zaidi ya 50k ya hizo hela, (200,100,50 na 500)
Na sina pa kuzipeleka, nafurahi tu kuziona, sasa na mwingine na mwingine,

Mm nikipata chenji kama hizo nikaingia nazo home, bas hesabu hizo zimetoka kwa mzunguko wa pesa, mana nitaweka kwa kopo langu
 
Hali imekuwa tete sasa hivi hazionekani mtaani
 
Kumekuwa na uhaba mkubwa sana wa sarafu tajwa hapo juu sijajua kama bot kama msimsmizi wa hizi pesa anafahamu hili au waziri wa fedha alitolee ufafanuzi maana kina dalili ya vitu vidogo vidogo hata vikubwa kupanda bei

Wafanya biashara mfano daladala wameathirika na hili

Wafanyabiashara wa maduka mfano ya bidhaa za nyumbani wanakulazimisha uchukue pipi ku balance hesabu zao

Shida ipo wapi serikali?
 
Back
Top Bottom