Uchaguzi 2020 Ushauri wangu kwa CHADEMA

Uchaguzi 2020 Ushauri wangu kwa CHADEMA

Mpangawangu

JF-Expert Member
Joined
Mar 5, 2014
Posts
887
Reaction score
965
Mnafanya vizuri kampeni za Urais lakini yafuatayo ni mapungufu niliyojionea kwa macho na mengine nimefuatilia kupitia mitandao.

1. Vijana wa CHADEMA wamepoa mitandaoni, wanashindwa kwa mbali sana na vijana wa ACT-Wazalendo, yaani Mkutano mkubwa wa Lissu unafanyika hakuna TV hata moja inayorusha mkutano na hata hao TBC wakirusha wanafanya hujma za wazi.

Njia pekee ni kujikita kwenye mitandao ya kijamii hasa YouTube, Instagram, Facebook na Twitter.

Undeni timu ya vijana ambao wapo tayari, msiwaache aki na Malisa na wengine mnaowafahamu, wafanye kazi ifuatayo.
1Kila mkutano wa Lissu mnapo jenga jukwaa wekeni minara walau minne ya watu wenu wa Camera kusimama ili waweze kupata picha nzuri za mahudhurio ya watu.

2. Tumieni online tv, live stream kuhakikisha Lissu anakuwa live muda wote(nunueni Camera za kueleweka na kama hamna pesa ombeni mchango) haizidi mil 10 kupata vifaa vya kawaida vya kurushi mkutano, mbona wenzenu ACT wanaweza na picha inakuwa bora? Wao wamewezaje wakati ni chama kidogo halafu chama kikuu cha upinzani mnashindwa? Onesheni ukubwa wenu sasa.

3. Undeni kikosi kazi cha kuwalisha watu kwenye mitandao kwa kukata clip fupifupi zinazofafanua hoja flani hizo ziende tweeter, Instagram na Facebook.

4. Wakati huo undeni vikosi kazi vya nyumba kwa nyumba viende kufafanua hoja za Lissu kw wazee na wale wasiohudhuria mikutano

Jambo moja mnatakiwa kujua, Masoko ni platform nzuri kwa Chadema kujijenga, wafanya biashara kwenye masoko Mengi ya Tanzania wanawaelewa sana, wanawafuatilia kila mnapoenda, na kwakuwa si rahisi kuacha biashara zao,wao wanawaangalia YouTube, wakiwakosa YouTube wanaumia sana.

Wafanyabiashara sokoni wanawasaidia sana kuwakampenia kwa wateja wao, kila mteja akifika kununua chochote lazima aondoke na ujumbe, namna ya kuwa feed cha kuongea na wateja ni kuwa active mitandaoni kama anavyofanya Kigogo, amabe kila baada ya dk 2 lazima aandike chochote ili kuwaburudisha wafuasi wake.

Chadema mnakwama wapi? Au account zenu zimedululiwa?

Mwisho, link inayoonesha live mkutano isambazeni kila kichochoro ili hata mshindani wenu awaangalie.

Sio mnafanya mkutano leo halafu YouTube mnaweka kesho yake.
 
Back
Top Bottom