Kabla ya kuingia kwenye mapambano makali ya kudai maboresho ya Katiba na Sheria bora za Uchaguzi, nadhani CHADEMA wangefanya yafuatayo kwanza:-
1. Iandaliwe orodha ya maboresho muhimu ya Katiba na sheria yanayotakiwa kufanyiwa kazi kabla ya uchaguzi.
Baada ya kuandaliwa, hiyo orodha ya maboresho ifikishwe kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili atafute muda wa kukaa pamoja na kufikia makubaliano.
2. Kama Rais atakubali kukaa mezani kuyajadili na kufikia mwafaka, basi kuwepo na ratiba maalumu itayoongoza majadiliano hayo.
3. Ikiwa watawala hawatakuwa tayari kufanya maboresho ya Katiba na Sheria bora za Uchaguzi, CHADEMA wachukue hiyo orodha ya maboresho pamoja na muhtasari wa hali halisi ya chaguzi za mwaka 2019, 2020 na 2024 na kuandaa malalamiko maalumu dhidi ya utawala na kuyafikisha katika Taasisi zote ndani na nje ya Nchi ikiwa ni pamoja na mabalozi wote, Jumuiya zote na zile za kimataifa na za kikanda, vyombo vyote vya habari ndani na nje ya Nchi na mitandao yote ya mawasiliano Duniani na kwa Watanzania wote pamoja na mashirika mbalimbali ya Dini na kwa viongozi wa Dini ndani na nje ya Nchi.
4. Baada ya kuwa Dunia imefahamu kwa kina nini kilifanyika wakati wa uchaguzi wa mwaka 2019, 2020 na 2024 na kwamba CHADEMA wameandaa Rasimu ya maboresho ya Katiba na Sheria za Uchaguzi ili yaliyotokea miaka hiyo ya uchaguzi yasitokee tena na watawala wamekataa, hapo ndipo zianze kuchukuliwa hatua zozote zile madhubuti zitakazosaidia kushinikiza upatikanaji wa Katiba mpya na Sheria bora za Uchaguzi kwa ustawi Nchi yetu.
NB:- Mapambano ya kudai haki ni magumu sana ikizingatiwa kuwa watu wanapambana na watawala wanaomiliki vyombo vyote vya ulinzi na usalama, kwa hiyo kabla ya kuanza mapambano ni vema kuahana na nyonga kwanza.
Nawasilisha.
Pia soma: Pre GE2025 - Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025